PSLE NECTA Results - Matokeo ya darasa la saba miaka yote kimkoa

NECTA - Matokeo ya darasa la saba 2021 - PSLE Results 2021/2022 (New Updates)

necta yatangaza - Matokeo ya darasa la saba 2021 -  matokeo ya darasa la saba 2021  yatangazwa leo - shule walizopangiwa 2021/2022


MTIHANI  WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI DARASA LA SABA 2021

TAREHE YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2020.

KUANZA - 07.10.2020 - JUMATANO. Exam Timetable

KUMALIZA - 08.10.2020 - ALHAMISI. Ratiba ya mtihani

Tanzania standard seven national examination results 2021/2022 - Jinsi ya kupata matokeo ya darasa la saba mwaka 2021 - 2022 kwenye mtandao.

NECTA PSLE EXAMS PAST PAPERS QUESTIONS & ANSWERS - MASWALI NA MAJIBU DARASA LA SABA.


TO VIEW PSLE RESULTS 2020 CHOOSE THE REGION (KUANGALIA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2020/2021 NECTA - CHAGUA MKOA) 

MATOKEO LA SABA (PSLE Results) 2020

PSLE NECTA Results- Matokeo ya darasa la saba Mkoa wa SONGWE

Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba 2020


MPANGILIO WA MIKOA KWA UBORA WA UFAULU MTIHANI WA DARASA LA SABA (PSLE) 2019/2020


MPANGILIO WA HALMASHAURI KWA UBORA WA UFAULU MTIHANI WA DARASA LA SABA (PSLE) 2019/2020


MATOKEO YA DARASA LA NNE 2020/2021


RATIBA YA MIHULA YA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KWA MWAKA 2020


RATIBA YA MTIHANI WA DARASA LA SABA MWAKA 2019

standard seven national examination results 2020


MATOKEO YA DARASA LA SITA 2020>>Mtihani wa darasa la saba Utaanza Jumatano 11/09/2019 na kumalizika Alhamisi 12/09/2019 >>NECTA PSLE RESULTS 2019/2020


RATIBA YA MTIHANI WA DARASA LA SABA
Ratiba Mtihani wa darasa la saba 2019 - (PSLE Exam Timetable 2019) 
Ratiba ya Mtihani wa darasa la saba mwaka 2018 (PSLE Exam Timetable 2018)Ratiba ya Mtihani wa darasa la saba mwaka 2017 (PSLE Exam Timetable 2017)

TOP 10 SECONDARY SCHOOLS IN TANZANIA 2019 - Shule bora za sokondari.


FOMATI YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI (Pata matokeo ya darasa la saba 2020 necta)

KISWAHILI

Fomati hii ya somo la Kiswahili haitofautinani na ile ya mwaka 2011 kimaudhui bali kuna mabadiliko kimuundo ambapo mtihani utakuwa na maswali 40 ya kuchagua na maswali matano (5) ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi.
Muundo wa Mtihani
  • Mtihani wa Kiswahili utakuwa na sehemu A, B, C, D na E. Sehemu A itahusisha mada ya Sarufi, sehemu B itahusisha mada ya Lugha ya Kifasihi, sehemu C itahusisha mada ya Ushairi, sehemu D itahusisha Utungaji au Uandishi na sehemu E itahusisha mada ya Ufahamu.
  • Mtihani utakuwa na jumla ya maswali arobaini na tano (45) na watahiniwa watatakiwa kujibu maswali yote.
  • Katika sehemu A, B, C na D kila swali litakuwa na alama moja (1). Aidha, katika sehemu E kila swali litakuwa na alama mbili (2).
  • Swali la 1 – 40 yatajibiwa katika fomu ya OMR kwa kutumia kalamu ya penseli ya HB na swali la 41 – 45 yatajibiwa katika sehemu iliyoachwa wazi katika karatasi ya maswali kwa kutumia kalamu ya wino wa bluu au mweusi.
  • Muda wa kufanya mtihani utakuwa saa 1:30 ambapo watahiniwa wasioona watafanya mtihani kwa muda wa saa 1:45.
Sehemu A: Sarufi
  • Sehemu hii itakuwa na maswali ishirini (20) ya kuchagua Maswali yatajikita katika kubainisha aina za maneno, kutumia kwa usahihi aina mbalimbali za maneno, miundo ya sentensi na nyakati mbalimbali.
  • Mtahiniwa atatakiwa kujibu maswali yote katika sehemu hii kwa kuchagua jibu sahihi kutoka katika chaguzi A, B, C, D na E.
Sehemu B: Lugha ya Kifasihi
  • Sehemu hii itakuwa na maswali kumi (10) ya kuchagua.  Mtahiniwa atatakiwa kujibu maswali yote.
  • Maswali katika sehemu hii yatakuwa ya kuchagua jibu sahihi kutoka katika chaguzi A, B, C, D na E.
  • Maswali  yatajikita katika mada ya methali, nahau na vitendawili.
Sehemu C: Ushairi
  • Maswali katika katika sehemu hii yatakuwa ya kuchagua jibu sahihi kutoka katika chaguzi A, B, C, D na E.
  • Maswali hayo hayo yatajikita zaidi katika mada ya ushairi na tenzi
Sehemu D: Utungaji/Uandishi wa Habari na Barua
  • Sehemu hii itakuwa na sentensi nne (4) zilizochanganywa ambapo mtahinwa atatakiwa kuzipanga katika mtiririko unaoleta maana.
  • Maswali haya yatakuwa ya kuchagua sentensi sahihi kutoka katika chaguzi A, B, C na D.
  • Mtahiniwa atatakiw akujibu maswali yote.
Sehemu E: Ufahamu
  • Sehemu hii itakuwa na maswali matano (5) na mtahiniwa atatakiwa kujibu maswali yote.
  • Maswali yote yatakuwa ya kujaza nafasi iliyoachwa wazi.
  • Maswali yatajikita katika ufahamu wa kusoma habari.
Mada Zitakazotahiniwa
  • Sarufi
  • Lugha ya kifasihi
  • Ushairi
  • Utungaji/Uandishi wa Barua/Uandishi wa Habari 5.5 Ufahamu

ENGLISH LANGUAGE

Examination Rubric
  • The English language Examination consists of sections A, B, C and D with a total of 45 questions. Candidates will be required to answer  all questions.
  • Section A will comprise of Grammar, Section B Vocabulary, Section C Composition and Section D Comprehension.
  • Questions 1 to 40 will carry one (1) mark each, while questions 41 to 45 will carry two (2) marks each. The whole examination will have a total of fifty (50) marks.
  • In question 1 – 40 candidates will use the OMR forms to respond using HB pencil while in question 41 – 45 candidates will give their answers in the spaces provided in the question paper using blue or black ink pen.
  • The duration of the paper will be 1:30 Hours. Visual impaired candidates will take the examination for 1:45 Hours.
Section A:  Grammar
  • This section will consist of thirty (30) questions out of which ten (10) questions will be set from the topic of Tenses and 20 questions from other forms of grammar.
  • Candidates will be required to answer all the questions by choosing the correct answer from the given alternatives A, B, C, D and E.
Section B: Vocabulary
  • This section will consist of six (6) multiple choice questions and will test the use of vocabulary in different context.
  • Candidates will be required to answer all the questions by choosing the correct answer from the given alternatives A, B, C, D and E.
Section C: Composition
  • This section will comprise of four (4) mixed/jumbled sentences. The candidate will be required to arrange the sentences logically so as to make a good composition.
  • The sentences will be arranged using letters A to D.
Section D: Comprehension
  • This section will consist of a short passage which will be followed by five (5) short answer questions.
  • Candidates will be required to read the passage and answer all the questions the space provided.

  • Tenses
  • Other forms of Grammar 5.3 Vocabulary
  • Composition
  • Comprehension

MAARIFA YA JAMII (URAIA, HISTORIA NA JIOGRAFIA)

Muundo wa Mtihani
  • Mtihani wa Maarifa ya Jamii utakuwa na sehemu A na  B zenye kupima mada kutoka masomo ya  Uraia, Historia  na Jiografia.
  • Sehemu A itakuwa na maswali 40 ya kuchagua na sehemu B itakuwa na maswali 5  ya majibu mafupi ambapo swali moja ni kutoka katika somo la uraia, maswali mawili kutoka somo la Historia na maswali mawili mengine kutoka somo la Jiografia. Hivyo, kufanya jumla ya maswali 45 katika mtihani huu.
  • Mtahiniwa atatakiwa kujibu maswali yote ambapo, swali la 1 -40 atajibia katika fomu ya OMR kwa kutumia kalamu ya penseli ya HB na swali 41 – 45 atajibia katika sehemu iliyoachwa wazi katika karatasi ya maswali kwa kutumia kalamu ya wino wa bluu au mweusi.
  • Muda wa kufanya mtihani utakuwa saa 1:30 ambapo watahiniwa wasioona watafanya mtihani kwa muda wa saa 1:45.
Sehemu A
  • Sehemu A itakuwa na vipengele vitatu; kipengele cha I Uraia, cha II Historia na cha III Jiografia.
Kipengele I: Uraia
  • Kipengele hiki kitakuwa na jumla ya maswali 12 ya kuchagua jibu sahihi katika katika chaguzi A, B, C, D na E.
  • Mtahiniwa atatakiwa kujibu maswali yote.
  • Kila swali litakuwa na alama moja (1) hivyo kufanya kipengele hiki kuwa na jumla ya alama 12.
Kipengele II:  Historia
  • Kipengele hiki kitakuwa na jumla ya maswali 14 ya kuchagua jibu sahihi katika katika chaguzi A, B, C, D na E.
  • Mtahiniwa atatakiwa kujibu maswali yote.
  • Kila swali ilitakuwa na alama moja (1) hivyo kufanya kipengele hiki kuwa na jumla ya alama 14.
  • Kipengele hiki kitakuwa na jumla ya maswali 14 ya kuchagua jibu sahihi kutoka katika chaguzi A, B, C, D na E.
  • Mtahiniwa atatakiwa kujibu maswali yote.
  • Kila swali ilitakuwa na alama moja (1) hivyo kufanya kipengele hiki kuwa na jumla ya alama 14.
Sehemu  B
  • Sehemu hii itakuwa na jumla ya maswali matano (5) ya majibu mafupi kutoka katika mada mbalimbali za somo la Uraia, Historia, na Jiografia kwa uwiano wa; Uraia swali moja (1), Historia maswali mawili (2) na Jiografia maswali mawili (2).
  • Swali moja (1) la somo la Uraia litakuwa la majibu mafupi kuhusu dhana mbalimbali za somo hilo. Maswali mawili (2) ya somo la Historia yatakuwa ya majibu mafupi na yatatokana na dhana mbalimbali za somo hilo na maswali mawili (2) ya Jiografia yatahusu dhana mbalimbali kama vile michoro, ukokotoaji, tafsiri ya Picha na Ramani na uchambuzi wa takwimu.
Mada Zitakazotahiniwa
Mada zitakazopimwa katika mtihani wa Maarifa ya Jamii ni kama ifuatavyo:
Uraia
  • Uongozi
  • Alama za shule na za taifa
  • Misingi ya demokrasia
  • Ulinzi na Usalama
  • Utamaduni wetu
  • Uchumi wetu
  • Ushirikiano baina ya Tanzania na mataifa mengine
Historia
  • Elimu ya familia
  • Chimbuko na mabadiliko ya binadamu
  • Mahusiano ya Watanzania na jamii za kigeni 5.2.4 Tanzania huru
  • Uvamizi wa kimataifa
  • Afrika huru
Jiografia
  • Mazingira
  • Picha
  • Ramani
  • Usomaji wa ramani 5.3.5 Mfumo wa Jua
  • Majanga
  • Maji

HISABATI (std seven 2020)

Muundo wa Mtihani
  • Mtihani utakuwa maswali 45 yenye sehemu A na B. Mtahiniwa anatakiwa kujibu maswali yote katika sehemu A na B.
  • Sehemu A itakuwa na maswali 40 ambapo mtahiniwa atatakiwa kukokotoa na kisha kuchagua jibu sahihi kati ya chaguzi A, B, C, D na E na kujaza jibu hilo sahihi katika fomu ya OMR kwa kutumia kalamu ya penseli ya HB.  Kila swali katika sehemu hii litakuwa na alama moja (01) hivyo kufanya jumla ya alama 40 katika sehemu hii.
  • Sehemu B itakuwa na maswali matano yenye alama 02 kwa kila swali ambayo mtahiniwa anatakiwa kukokotoa kwa kuonesha njia au kuchora na kuandika jibu kwenye eneo lililotengwa katika karatasi ya maswali kwa kutumia kalamu ya wino wa bluu au mweusi. Sehemu B itakuwa na jumla ya alama 10.
  • Maswali ya sehemu A yatatoka katika maeneo makuu yafuatayo: Matendo ya Hisabati – maswali 22, maumbo maswali 9 na mafumbo maswali 9. Aidha, maswali ya sehemu B yatatoka katika maeneo makuu yafuatayo: Matendo ya    Hisabati – swali moja (01), maumbo maswali mawili (02) na mafumbo maswali mawili (02).
  • Muda wa kufanya mtihani utakuwa saa 2:00 ambapo watahiniwa wasioona watafanya mtihani kwa muda wa saa 2:40.
Mada za Mtihani
  • Namba nzima
  • Sehemu
  • Fedha
  • Jometri
  • Vipimo
  • Namba za Kirumi
  • Takwimu
  • Vipeo na Vipeuo 5.9 Desimali
  • Asilimia
  • Aljebra
  • Majira ya Nukta 5.13 Namba Kamili
SAYANSI Muundo wa Mtihani
  • Mtihani wa Sayansi utakuwa na sehemu A na  B  zitakazopima mada mbalimbali.  Jumla ya maswali yatakuwa arobaini na tano (45). Mtahiniwa atatakiwa kujibu maswali yote.
  • Sehemu A itakuwa na maswali arobaini (1 - 40) ya kuchagua jibu sahihi kutoka katika chaguzi A, B, C, D na E. Kila swali litakuwa na alama moja (01) hivyo kufanya jumla ya alama 40 katika sehemu hii.
  • Sehemu B itakuwa na maswali matano (41 - 45) kutoka katika mada mbalimbali.  Maswali hayo yatahusu kujibu kwa ufupi dhana mbalimbali zitakazoulizwa, kuchora au kujaza sehemu za michoro, ukokotoaji na uchambuzi wa takwimu za kisayansi. Kila swali litakuwa na alama mbili (02) hivyo kufanya jumla ya alama kumi (10) katika sehemu hii.
  • Mtahiniwa atatakiwa kujibu swali la 1 – 40 katika fomu ya OMR kwa kutumia kalamu ya penseli ya HB na swali la 41 – 45 katika sehemu iliyoachwa wazi katika karatasi ya maswali kwa kutumia kalamu ya wino wa bluu au mweusi.
  • Muda wa kufanya mtihani utakuwa saa 1:30 ambapo watahiniwa wasioona watafanya mtihani kwa muda wa saa 1:45.
Mada Zitakazotahiniwa
  • Viumbe hai
  • Mahitaji muhimu kwa afya na uhai
  • Afya, huduma za afya na njia za kujikinga na magonjwa
  • Huduma ya kwanza
  • Virusi vya UKIMWI na UKIMWI
  • Mabadiliko ya Violwa, Hali na Matukio
  • Nishati, mashine na kazi
  • Mbinu na taratibu za kisayansi

MATOKEO DARASA LA SABA 2020 ZANZIBAR - NECTA PSLE RESULTS 2020 ZANZIBAR 

psle results 2020 - matokeo darasa la saba 2020 necta

matokeo ya darasa la saba 2020 na shule walizopangiwa