Matokeo ya Darasa la Sita Mwaka 2020 - Zanzibar
BARAZA LA MITIHANI LA ZANZIBAR - ZANZIBAR EXAMINATIONS COUNCIL
MTIHANI WA TAIFA DARASA LA SABA (NECTA) MASWALI NA MAJIBU
STANDARD SIX NATIONAL EXAMINATIONS RESULT 2020
TAARIFA YA MATOKEO YA MITIHANI YA TAIFA YA MWAKA 2020
Taarifa ya matokeo ya darasa la nne 2020
Taarifa ya matokeo ya darasa la nne 2020
Taarifa ya matokeo ya darasa la nne 2020
Taarifa pia inajumuisha watahiniwa 10 bora kitaifa na shule 10 bora kitaifa
ISOME HAPA >>TAARIFA YA MATOKEO YA MITIHANI YA TAIFA YA MWAKA 2020
Matokeo ya Darasa la Sita 2018/2019 - Zanzibar
Matokeo ya Darasa la Sita Mwaka 2017
DARASA LA SITA 2019
Uandikishaji wa watahiniwa wa Mtihani wa Taifa wa Darasa la Sita ulifanyika katika Skuli 380, kati ya Skuli hizo, Skuli 273 ni za Serikali na 107 ni za Binafsi. Kuna ongezeko la Skuli 07 sawa na asilimia 1.8 ikilinganishwa na Skuli zilizoandikishwa mwaka 2018. Watahiniwa 32,308 waliandikishwa kufanya mtihani huo kati yao Wanawake ni 16,940 na asilimia 52.4 na Wanaume ni 15,368 sawa na asilimia 47.6. Idadi hii imepungua kwa watahiniwa 4,404 sawa na asilimia 12 ikilinganishwa na watahiniwa 34,444 walioandikishwa mwaka 2018. Watahiniwa 31,185 walifanya mtihani huo sawa na asilimia 96.5 ambapo wanawake ni 16,633 sawa na asilimia 53.3 na wanaume 14,552 sawa na asilimia 46.7. Aidha watahiniwa 1,123 sawa na asilimia 3.5 hawakufanya Mtihani huo kutokana na sababu mbali mbali zikiwemo utoro na ugonjwa.
MATOKEO 2019
Ufaulu unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 30,419 sawa na asilimia 97.5 kati ya 31,185 waliofanya mtihani huu wamefaulu kwa madaraja ya A, B, C na D na watahiniwa 766 sawa na asilimia 2.5 hawakufaulu.
Ufaulu huo umepanda kwa asilimia 1.2 ukilinganishwa na ufaulu wa asilimia 96.3 wa mwaka 2018.
Idadi ya watahiniwa waliofaulu ambao wenye sifa ya kuendelea na masomo ya Kidato cha kwanza katika madarasa ya Vipawa (194), Michepuo (1,508) na Sekondari za kawaida (28,717) imeongezeka kwa mwaka 2019. Aidha Ubora wa ufaulu unaonesha kuwa idadi ya watahiniwa waliofaulu kwa Daraja A, B na C umepanda kwa kuwa na asilimia 41.3 ikilinganishwa na asilimia
37.4 ya mwaka 2018.
WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI ZAIDI KITAIFA 2019
Matokeo yanaonesha kuwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi Kitaifa kwa madarasa yote ya mitihani ni:-
- Zainab Hussein Kurwa kutoka Skuli ya Upendo (Darasa la Nne).
- Ummu-Kulthum Juma Ali Skuli ya Miti Ulaya (Darasa la Sita).
- Amina Hassan Khatib kutoka Skuli ya Lumumba (Kidato cha Pili).
SKULI ZILIZOFANYA VIZURI ZAIDI 2019
Skuli zilizofanya vizuri zaidi Kitaifa kwa Darasa la Nne ni Skuli ya Great vision na Upendo nursury & primary school.
Skuli zilizofanya vizuri zaidi Kitaifa kwa Darasa la Sita ni Skuli ya Feza na Evergreen.
Skuli zilizofanya vizuri zaidi Kitaifa kwa Kidato cha Pili ni Skuli ya
Lumumba na Utaani B.
UFAULU WA KIWILAYA 2019
Kwa Mtihani wa Darasa la Nne, Wilaya ya Magharibi “B’’ inaongoza katika ufaulu wa ujumla kwa kupata asilimia 90.5 ikifuatiwa na Wilaya ya Mjini yenye ufaulu wa asilimia 89.9. Aidha, Wilaya ya Mkoani ni ya mwisho kwa kupata asilimia 67.3.
Kwa Darasa la Sita, Wilaya zote zimefanya vizuri na ufaulu wao umepanda ambapo Wilaya ya Micheweni inaongoza kwa Skuli za Serikali kwa kufanya vizuri zaidi kwa kupata asilimia 98.9 ambapo Wilaya ya Kati ni ya mwisho yenye asilimia 94.8.
Kwa upande wa Mtihani wa Kidato cha Pili, Wilaya zote zimefanya vizuri ambapo Wilaya ya Micheweni inaongoza kwa kupata asilimia 83.4 na Wilaya ya Kaskazini ‘B’, Wilaya ya Kati na Wilaya ya Kusini zinaonekana kuwa ni za mwisho kwa kupata asilimia 62.2, 62.4 na 63.1.
OTHER EXAMINATION RESULTS
Matokeo ya Darasa la Nne Mwaka 2018
Matokeo ya Darasa la Nne Mwaka 2017
Malengo ya Elimu Zanzibar
- Kukuza na kuendeleza maadili ya utamaduni, itikadi, desturi za Watanzania ili kuimarisha umoja na utambulisho wa kitaifa.
- Kukuza upatikanaji na matumizi sahihi ya ujuzi na maarifa kwa ajili ya maendeleo endelevu ya jamii.
- Kuwawezesha raia wote kuelewa na kuheshimu misingi ya katiba,wajibu na haki za binaadamu.
- Kukuza uelewa wa matumizi sahihi, usimamizi na uhifadhi wa mazingira.
- Kuongeza upendo, heshima na nidhamu katika kazi, ili kuongeza ufanisi
- Kuhamasisha ufuataji wa kanuni, kuendeleza amani na uvumilivu, upendo, haki, uelewa wa haki na wajibu wa binadamu, umoja wa kitaifa, ushirikiano wa kimataifa kama unavyoelezwa katika mikataba ya msingi ya kimataifa.