Kujiunga kidato cha kwanza |
WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KUDATO CHA KWANZA 2018/2019, FORM ONE SELECTION 2018/2019, SELECTION DARASA LA SABA 2016/2017.
waliochaguliwa kidato cha kwanza 2018/2019
WE WISH YOU A MERRY XMASS! - ALL THE STUDENTS!
majina ya waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2019
Jafo atangaza waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2019 Leo tarehe 13/12/2018 - Form One Selection 2019 - New Updates
Serikali yatangaza majina ya waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018.
Wanafunzi 650,862 kati ya 662,035 waliofaulu wamechaguliwa katika awamu ya kwanza, hii ikiwa ni sawa na asilimia 98.31
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo amesema kati ya wanafunzi 662,035 waliofaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi wanafunzi 650,862 sawa na asilimia 98.31 wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza mwaka 2018
Akitangaza matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 idadi ya wanafunzi mwaka huu imeongezeka kwa wanafunzi 124,209 ambapo ni sawa na asilimia 23.58 ikilinganishwa na wanafunzi 526,653 waliochaguliwa awamu ya kwanza kuingia kidato cha kwanza mwaka 2017.
Wanafunzi 1912 wenye uhitaji maalum (pupils with special needs) waliofaulu mitihani ya darasa la saba wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwaka 2018 kwenye shule za sekondari za Serikali.
Mhe. Jafo amefafanua kuwa wanafunzi 11,173 sawa na asilimia 1.69 ya waliofaulu hawakupata nafasi ya kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza ya uchaguzi kutokana na uhaba wa miundombinu ya elimu hususani vyumba vya madarasa kwenye baadhi ya Halmashauri.
Halmashauri ambazo zimeshindwa kuwapangia wanafunzi wote waliofaulu nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza ni Halmashauri za Lindi wanafunzi (80) Mbeya (207),Halmashauri ya Jiji la Mbeya ( 1,227), Mbarali (1,578), Kalambo (166), Nkasi (1,318), Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga (1,054), Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga (1,553), Babati (581). Hanang (687), Mpanda (262), Nsimbo (714), Halmashauri ya Mji wa Bariadi (369) na Halmashauri ya Wilaya ya Busega (1,207).
Mhe. Jafo amewaagiza Wakuu wa Mikoa ambayo haijakamilisha ujenzi wa miundombinu hasa ya vyumba vya madarasa kuhakikisha wanakamilisha hadi kufikia mwezi februari, 2018 ili wanafunzi watakaochaguliwa kwenye awamu ya pili wapate nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018.
“Lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa darasa la saba wanapata nafasi ya kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza maelekezo yametolewa kwa wakuu wa mikoa kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanapata nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2018” Amesema Jafo
shule walizopangiwa kidato cha kwanza 2018 (Video)
WHAT DOES IT TAKE TO BECOME A SUCCESSFUL STUDENT?
Darasa la Saba waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2017.
Matokeo Yote Ya Mitihani - One Spot For All The Examination Results
Selection kidato cha kwanza 2017
Biology Lessons & Notes - FORMS I, II, III, IV
94.8% Wachaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza 2017
WANAFUNZI 526,653 sawa na asilimia 94.8 ya waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka huu, wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani katika shule za sekondari za serikali katika awamu ya kwanza huku 28,638 wakishindwa kupangiwa shule katika awamu ya kwanza.Kati ya wanafunzi hao, wasichana ni 268,052 sawa na asilimia 94.5 ya wasichana waliofaulu na wavulana ni 258,601 sawa na asilimia 95.2 ya wavulana waliofaulu. Wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka 2016 walikuwa 795,739, huku 244 wakifutiwa matokeo ya mtihani kutokana na udanganyifu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene alisema wanafunzi waliochaguliwa wamegawanyika katika makundi manne likiwemo:-
- Shule za bweni kwa wenye ufaulu mzuri ambao waliochaguliwa ni 900 wavulana 480 na wasichana 420.
- Shule za bweni za ufundi waliochaguliwa - 1,005.
- Shule za bweni kawaida - 780.
- Shule za bweni kwa wenye ulemavu - 723.
- Shule za kutwa wanafunzi waliochaguliwa - 523,245.
Ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.52 ukilinganisha na asilimia 67.84 kwa mwaka 2015.
Simbachawene alisema katika uchaguzi huo, wanafunzi 28,638 hawakuchaguliwa katika awamu ya kwanza, na kuitaja mikoa ambayo wanafunzi wamebaki ni Dar es Salaam (18,820), Arusha (4,752), Songwe (1,465), Kigoma (1,208), Manyara (1,141), Lindi (608), Mbeya (406) na Katavi (238).
Aidha, waziri huyo alisema kati ya wanafunzi 1,060,588 walioanza darasa la kwanza 2010, wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka 2016 ni 795,739 sawa na asilimia 75 ya wanafunzi walioandikishwa wakiwemo wasichana 422,562 sawa na asilimia 53.1 na wavulana 373,177 sawa na asilimia 46.9 ya waliosajiliwa.
Akizungumzia udanganyifu, alisema watawavua madaraka kwa waliokuwa waratibu elimu kata na walimu wakuu, kuwashitaki mahakamani na kupeleka mashauri yao Tume ya Utumishi ya Walimu, baada ya udanganyifu kuongezeka ambako watahiniwa 244 wamefutiwa matokeo mwaka 2016 ikilinganishwa na wanane wa mwaka jana.
SUCCESS JOURNEY - What Most Successful people do.
Alizitaja shule zilizohusika kwenye udanganyifu huo ni Shule ya Tumaini na Little Flower za Sengerema mkoani Mwanza, Mikahamakumi iliyopo Sikonge, Tabora ambazo ni za binafsi, wakati za serikali ni Kondi Kasandalala iliyopo Sikonge, Tabora, Qash iliyopo Babati na St Getrude iliyopo Madaba mkoani Ruvuma.
Aidha, alisema 10 bora za serikali ni Kazunzu iliyopo Halmashauri ya Buchosa (Mwanza), Mwanahegele ya Maswa (Simiyu), Huruma ya Mbinga (Ruvuma), Kabanga ya Ngara (Kagera), Butumba B (Jiji Mwanza), Masoko ya Kilwa (Lindi), Lyambamgongo ya Bukombe (Geita), Kilimani ya Geita Vijijini, Magufuli ya Chato na Nkome ya Geita Vijijini, Geita.
Alisema shule 10 zilizofanya vibaya ni Chohelo ya Mvomero (Morogoro), ambayo ni ya mwisho kitaifa ikifuatiwa na shule za Iloliento, Longido (Arusha), Mwalebi na Nchilila Meatu (Simiyu), Magingi ya Mvomero, Kilole ya Lushoto, Tanga, Zege ya Korogwe, Tanga na shule tatu za Lubchi, Kitengo na Mgata za Morogoro vijijini.