SFNA 2017 EXAM TIMETABLE - TIMITABLE DARASA LA NNE 2017
NECTA SFNA 2017 TIMETABLE.pdf
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA - NECTA
RATIBA YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE - (STANDARD FOUR NATIONAL ASSESSMENT-SFNA) NOVEMBA 2017
Shule Bora Tanzania - TOP 10 Best Secondary Schools In Tanzania - New Update
Standard Seven Exams Past papers (PSLE) - NECTA - New Updates
TAREHE NA SIKU | MUDA (SAA) | NAMBA MFICHO | SOMO |
22.11.2017 JUMATANO | 2:00 – 3:00 | 02 | ENGLISH LANGUAGE |
3:00 – 4:00 | MAPUMZIKO | ||
4:00 – 5:30 | 04 04E | HISABATI MATHEMATICS | |
6:30 – 8:30 | 6:30 – 8:30 | ||
5:30 – 7:30 | MAPUMZIKO | ||
7:30 – 8:30 | 05 05E | SAYANSI SCIENCE | |
23.11.2017 ALHAMISI | 2:00 – 3:00 | 01 | KISWAHILI |
3:00 – 4:00 | MAPUMZIKO | ||
4:00 – 5:00 | 03 03E | MAARIFA YA JAMII SOCIAL STUDIES | |
5:00 – 7:00 | MAPUMZIKO | ||
7:00 – 8:00 | 06 06E | STADI ZA KAZI, HAIBA NA MICHEZO VOCATIONAL SKILLS, PERSONALITY DEVELOPMENT AND SPORTS | |
8:00 – 9:00 | MAPUMZIKO | ||
9:00 – 10:00 | 07 07E | TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO (TEHAMA) INFORMATION AND COMMUNICATION TECHNOLOGY (ICT) |
SFNA 2017 EXAM TIMETABLE - TIMITABLE DARASA LA NNE 2017
MAELEKEZO MUHIMU - Darasa la nne timetable 2017
- Hakikisha kuwa unayo Ratiba ya Upimaji wa mwaka 2017 iliyoandaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania.
- Kabla ya kufungua bahasha yoyote yenye maswali ya upimaji, hakikisha kwamba unasoma jina la somo juu ya bahasha husika na kujihakikishia kuwa somo hilo ndilo linalostahili kufanyika wakati huo kulingana na Ratiba ya Upimaji.
- Endapo utata utajitokeza kati ya maelekezo yaliyomo ndani ya Karatasi ya Upimaji na Ratiba ya Upimaji, maelekezo yaliyomo katika karatasi ya upimaji husika ndiyo yatakayofuatwa.
- Watahiniwa WASIOONA na wale wenye UONI HAFIFU waongezewe MUDA WA ZIADA WA DAKIKA 10 KWA KILA SAA kwa upimaji wote isipokuwa DAKIKA 20 KWA KILA SAA kwa somo la Hisabati.
- Msimamizi wa watahiniwa WASIOONA awe mtaalamu mwaminifu aliye na uwezo wa kusoma maandishi na alama za ‘Braille’.
- Watahiniwa wenye UONI HAFIFU wapewe karatasi za upimaji na za kujibia zenye maandishi yaliyokuzwa, zilizoandaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania kwa matumizi yao.
- Karatasi zenye majibu ya watahiniwa wenye UONI HAFIFU zifungwe kwenye bahasha za pekee. Zisichanganywe na karatasi za watahiniwa wenye Uoni wa kawaida.
- Watahiniwa waelekezwe;
- Kuingia ndani ya chumba cha upimaji nusu saa kabla ya muda wa upimaji na watakaochelewa kwa zaidi ya nusu saa baada ya upimaji kuanza hawataruhusiwa.
- Kufuata maelekezo yote yatakayotolewa na wasimamizi wa upimaji.
- Kuandika jina kamili na namba ya upimaji kwa usahihi.
- Kutofanya mawasiliano ya maneno au kwa njia yoyote baina ya watahiniwa. Ikiwa mtahiniwa ana tatizo anatakiwa kunyoosha mkono ili kuomba msaada kwa msimamizi wa upimaji.
- Wakijihusisha katika udanganyifu watafutiwa matokeo yao ya upimaji.