Shule Zilizofanya Udanganyifu Kwenye Mtihani wa Darasa la 7 - 2016
HOW TO PLAN YOUR REVISION - Getting Ready For Exams
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
TAARIFA YA UFANYIKAJI WA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI (PSLE)
2016 MBELE YA WAANDISHI WA HABARI TAREHE 27/10/2016
UTANGULIZI
Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) 2016 ulifanyika Tanzania Bara tarehe 08 na 09 Septemba 2016 kwa amani na utulivu. Jumla ya shule 16,350 zilishiriki katika mtihani na watahiniwa 795,739 walisajili wa kufanya mtihani huo.
HALI YA UFANYIKAJI WA MITIHANI
Kamati za Mitihani za Mikoa/Manispaa/Halmashauri pamoja na wasimamizi wa mitihani walifanya kazi nzuri ya kuhakikisha Kanuni za mitihani zinazingatiwa ipasavyo. Aidha, Maafisa wa Baraza la Mitihani walifanya ufuatiliaji wa ufanyikaji wa mitihani katika shule mbalimbali kwa lengo la kujiridhisha na uzingatiaji wa Kanuni za uendeshaji wa mitihani ya Taifa.
Pamoia na kazi nzuri iliyofanywa na waendeshaji wa mitihani hii, kulijitokeza matukio machache ya udanganyifu yahyotanywa na baadhi ya Wasimamizi wa mitihani, Wamiliki wa Shule na Walimu Wakuu.
Biology Lessons & Notes - FORMS I, II, III, IV
MATUKIO YA UDANGANYIFU YALIYOJITOKEZA
Baadhi ya matukio ya udanganyifu yaliyojitokeza katika shule mbalimbali ni kama ifuatavyo:-
Na | Shule | Halmashauri na Mkoa | Maelezo ya Tukio | Wahusika walioshiriki Udanganyifu |
1 | Tumaini | Sengerema, Mwanza | Mmiliki wa Shule kuiba mtihani, kuandaa majibu ambayo watahiniwa waliandika kwenye sare za shule na kuyatumia ndani ya chumba cha mtihani |
|
2 | Little Flower | Srerengeti, Mara | Mwalimu Mkuu kuiba mtihani, kuandaa majibu na kumpa msimamizi mkuu pamoja na msimamizi ili wawapatie watahiniwa ndani ya chumba cha mtihani. Wakati wakitekeleza udanganyifu huo, msimamizi mmoja wa mtihani alikamatwa na Afisa wa Baraza aliyekuwa akifanya ufuatiliaji. |
|
3 | Mihamakumi | Sikonge, Tabora | Mwalimu Mkuu na walimu kufanyia watahiniwa mtihani ambapo walikamatwa na Maafisa wa TAKUKURU/Kamati ya Mitihani ya Mkoa. |
|
4 | Qash | Bahati, Manyara | Mwalimu alijificha chooni, kupokea maswali kutoka kwa watahiniwa, kuandaa majibu na kupatia mtahiniwa. |
|
5 | St Getrude | Madaba, Ruvuma | Mwalimu Mkuu na walimu kushirikiana na wanafunzi na kufanya udanganyifu kwa njia ya walimu kujificha mabwenini na kwenye nyumba ya mwalimu iliyopo karibu na chumba cha mtihani, watahiniwa kuomba ruhusa ya kwenda kujisaidia na kutoka na maswali kuwapelekea walimu na baadaye kufuata majibu na kusambaza ndani ya chumba cha mtihani. |
|
6 | Kondi, Kasandalala | Sikonge, Tabora | Wanafunzi kukutwa wana mfanano wa majibu ya kukosa usio wa kawaida, jambo linaloonesha kuwa walitumia chanzo kimoja cha majibu. |
|
HOW TO PREPARE PSYCHOLOGICALLY FOR EXAMS
HITIMISHO
Baraza la Mitihani la Tanzania limekwisha toa taarifa za waliohusika na kushiriki udanganyifu kwa mamlaka zao za utumishi ili wachukuliwe hatua kwa mujibu wa Kanuni za uturnishi wa umma, Aidha, Baraza la Mitihani halitamvurnilia mtumishi yeyote anayevunja kanuni na sheria za nchi kwa kuvuruga usimamizi wa mitihani ya Taifa.
Pamoja na kwamba Matokeo ya Darasa la saba yanatangazwa sasa, Baraza la Mitihani la Tanzania litafanya ufuatiliaji wa makusudi kwa wanafunzi waliofaulu na ambao watachaguliwa na rnarnlaka za uchaguzi kujiunga na Kidato cha Kwanza ili kujiridhisha na umahiri wao wa kuweza kumudu masomo ya Sekondari.