RATIBA YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI 2016 - PRIMARY SCHOOL LEAVING EXAMINATION TIMETABLE 2016
Biology Lessons & Notes - FORMS I, II, III, IV
HOW DO TOP STUDENTS STUDY?
HOW TO BECOME A SUCCESSFUL STUDENT
WINNERS ARE MADE, NOT BORN!
MAELEKEZO MUHIMU
1.Hakikisha kuwa unayo Ratiba ya Mtihani ya mwaka 2016 iliyoandaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania.
2.Kabla ya kufungua bahasha yoyote yenye maswali ya mtihani, hakikisha kwamba unasoma jina la somo juu ya bahasha husika na kujihakikishia kuwa somo hilo ndilo linalostahili kufanyika wakati huo kulingana na Ratiba ya Mtihani.
3.Endapo utata utajitokeza kati ya maelekezo yaliyomo ndani ya Karatasi ya Mtihani na Ratiba ya Mtihani, maelekezo yaliyomo katika karatasi ya mtihani husika ndiyo yatakayofuatwa.
4.Watahiniwa WASIOONA na wale wenye UONI HAFIFU waongezewe MUDA WA ZIADA WA DAKIKA 10 KWA KILA SAA kwa mtihani wa Kiswahili, English Language, Maarifa ya Jamii na Sayansi.
5.Watahiniwa WASIOONA na wale wenye UONI HAFIFU waongezewe MUDA WA ZIADA WA DAKIKA 20 KWA KILA SAA kwa mtihani wa Hisabati.
6.Msimamizi wa watahiniwa WASIOONA awe mtaalamu mwaminifu aliye na uwezo wa kusoma maandishi na alama za ‘Braille’.
7.Watahiniwa wenye UONI HAFIFU wapewe karatasi za mtihani na za kujibia zenye maandishi yaliyokuzwa, zilizoandaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania kwa matumizi yao.
8.Karatasi zenye majibu ya watahiniwa wenye UONI HAFIFU zifungwe kwenye bahasha za pekee. Zisichanganywe na karatasi za watahiniwa wenye Uoni wa kawaida.
KNOWLEDGE IS NOT POWER - IT IS A POTENTIAL POWER!
RATIBA YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI
(PRIMARY SCHOOL LEAVING EXAMINATION TIMETABLE)
SEPTEMBA 2016
TAREHE NA SIKU | MUDA (SAA) | NAMBA MFICHO | SOMO |
07.09.2016 JUMATANO | 2:00 – 3:30 | 01 | KISWAHILI |
3:30 – 4:30 | MAPUMZIKO | ||
4:30 – 6:30 | 04 04E | HISABATI MATHEMATICS | |
6:30 – 8:30 | MAPUMZIKO | ||
8:30 – 10:00 | 05 05E | SAYANSI SCIENCE | |
08.09.2015 ALHAMISI | 2:00 – 3:30 | 02 | ENGLISH LANGUAGE |
3:30 – 4:30 | MAPUMZIKO | ||
4:30 – 6:00 | 03 03E | MAARIFA YA JAMII SOCIAL STUDIES |