HESLB - UTOAJI WA MIKOPO KWA WANAFUNZI MWAKA 2016/2017

HESLB - UTOAJI WA MIKOPO KWA WANAFUNZI MWAKA 2016/2017


HOW DO TOP STUDENTS STUDY? 



Baada ya kukamilisha zoezi la Uchambuzi wa maombi ya Mikopo 88,163 yaliyopokelewa hadi kufikia tarehe 11 Agosti, 2016. Jumla ya Wanafunzi wapya 20,183 wamepangiwa Mikopo. Upangaji huu umezingatia vigezo vilivyomo katika mwongozo wa  utoaji wa mikopo uliopitishwa na Bodi ya wakurgezi na kuidhinishwa na wizaya ya elimu sayannsi na teknoloji. Vigezo hivyo ni pamoja na:

 I. Vipaumbele vya  kitaifa vinavyoendana na Mpango  wa Maendeleo  wa Taifa wa Miaka mitano, Dira ya Taifa ya  Maendeleo 2025 na Mafunzo ambayo yatazalisha wataalamu wanaokidhi mahitaji  ya kitaifa katika fani za kipaumbele ambazo ni;

• Fani za Sayansi za Tiba na Afya,
• Ualimu wa Sayansi na Hisabati,
• Uhandisi wa  Viwanda, Kilimo, Mifugo, Mafuta na Gesi Asilia,
• Sayansi Asilia, na
• Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu.

i. Uhitaji wa waombaji hususani wenye mahitaji  maalum kama vile ulemavu na uyatima
ii. Uhitaji wa waombaji wanaotoka katika familia zenye hali duni ya kimaisha
                                                                       

NOWanafunzi wapya waliopata mikopoJumla
1Wadahiliwa yatima waliopata mkopo873
2Wadahiliwa wenye ulemavu wa  viungo118
3Wadahiliwa  wahitaji wenye  mzazi mmoja3,448
4Wadahiliwa wahitaji waliofadhiliwa na taasisis mbali mbali87
5Wadahiliwa wahitaji wanaosoma  kozi  za kipaumbele6,159
6Wadahiliwa wahitaji wanaosoma kozi zingine 9,867
JUMLA20,183

Kiasi cha Fedha zinazohitajika
Bajeti iliyoidhinishwa kwa ajili ya ukopeshaji kwa mwaka wa fedha wa 2016/17 ni shilingi bilioni 483, kwa ajili ya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatao 25,717, na wanaoendelea na masomo wapatao 93, 295.

Hatua zinazofuata
I. Wanufaika wote wanaopungukiwa na sifa watachunguzwa kwa ajili ya kurekebishiwa au kuondolewa katika unufaika wa mkopo

II. Waombaji waliwasilisha taarifa zenye upungufu, taarifa zao zitahakikiwa, na wakibainika kuwasilisha taarifa za uongo watachukuiwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kufutiwa mikopo yao

III. Wanufaika wote watatakiwa kuhuisha taarifa kwa kujaza dodoso. Taarifa za ziada za kiuchumi za wazazi au walezi wao zitatumika kutanua uhalisia. Wale watakaokutwa na hadhi zisizo stahili, watapoteza sifa za kuendelea kupata mikopo na kulazimika kurejesha kiasi watakachokuwa wamepokea tayari.

IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MTENDAJI
HESLB - BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU



HOW TO SOLVE DIFFICULT PROBLES!



VIEW - HESLB - First Year Loan Allocations Status for 2016/17

Q & A - QUESTIONS AND ANSWERS