NACTE - TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA PILI (SECOND SELECTION) 2016/2017

NACTE - TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA PILI NA KUONGEZWA KWA MUDA WA KUFANYA MAOMBI KATIKA KOZI ZA CHETI NA DIPLOMA KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017, NACTE SECOND SELECTION 2016/2017 PUBLIC NOTICE.

 

KNOW THE BENEFITS OF "BEDTIME STUDY!"
Biology Lessons & Notes - FORMS I, II, III, IV 


NACTE SECOND SELECTION 2016/2017 IS NOW OFFICIALLY OUT! NACTE UTEUZI WA AWAMU YA PILI 2016/2017

TO VIEW  LOG IN WITH YOUR USER NAME & PASSWORD >>>>>>> NACTE CAS


Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS) kwa waombaji wa cheti na diploma umefunguliwa tena kuanzia 05/09/2016 mpaka 15/09/2016 kwa wale ambao hawakuchaguliwa katika kozi walizoomba pamoja na  kuruhusu waombaji wapya ambao kwa njia moja au nyingine hawakuomba udahili hapo awali.
GO TO NACTE CAS TO APPLY
 

 NACTE PUBLIC NOTICE

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba kudahiliwa katika kozi za cheti na diploma na Umma kwa ujumla kuwa lilifunga dirisha la maombi mnamo tarehe 13 Agosti 2016 ili kuruhusu uteuzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa kozi hizo. Uteuzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa cheti na diploma ulitarajiwa kutangazwa tarehe 31 Agosti 2016 lakini kwa sababu zilizo nje wa uwezo wetu umesogezwa mbele mpaka tarehe 5 Septemba 2016.


Baraza pia linapenda kutoa taarifa  kuwa Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS) kwa waombaji wa cheti na diploma utafunguliwa tena tarehe 5 Septemba 2016 hadi tarehe 15 Septemba 2016 ili kujaza nafasi za udahili zitakazokuwa wazi baada ya uchaguzi wa awamu ya pili. Hatua hii itawezesha kuruhusu machaguo mapya kwa wale ambao hawakuchaguliwa katika kozi walizoomba pamoja na  kuruhusu waombaji wapya ambao kwa njia moja au nyingine hawakuomba udahili hapo awali.

Baraza linaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kutokana na mabadiliko hayo.

Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
NACTE