JKT - WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JKT 2019

KIDATO CHA SITA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT 2019 - WALIOCHAGULIWA KWENDA JKT 2019

MAHITAJI YA KUJIUNGA NA JKT 2019 >> vifaa vya kwenda navyo jkt


MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JKT 2019


WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2019

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2019, kutoka shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria.

Sanjari na uchaguzi huo, JKT limewapangia makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 01 hadi 07 Juni 2019. Vijana waliochaguliwa wamepangiwa katika kambi za JKT Rwamkoma-Mara, JKT Msange-
Tabora, JKT Ruvu-Pwani, JKT Mpwapwa na JKT Makutupora-Dodoma, JKT Mafinga-Iringa, JKT Mlale-Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba-Tanga, JKT Makuyuni-Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa, na JKT Mtabila –Kigoma, JKT Itaka-Songwe, JKT Lua na JKT Milundikwa-Rukwa, JKT Nachingwea-Lindi.
Aidha, wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities) wanatakiwa kuripoti kambi ya JKT Ruvu iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.

JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo:-

  1. Bukta ya rangi ya ‘Dark Blue’ yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu.
  2. Raba za michezo zenye rangi kijani au blue.
  3. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.
  4. Soksi ndefu za rangi nyeusi.
  5. Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.
  6. Track suit ya rangi ya kijani au blue
  7. Nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.
Mkuu wa JKT anawakaribisha vijana wote waliochaguliwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.

Kuona orodha kamili ya majina ya vijana waliochaguliwa na maeneo ya makambi ya JKT waliyopangiwa bofya kwenye jina la kambi hapo chini
  1. JKT Rwamkoma-Mara

  2. JKT Msange-Tabora

  3. JKT Bulombora-Kigoma

  4. JKT Kanembwa-Kigoma

  5. JKT Mtabila –Kigoma

  6. JKT Ruvu-Pwani

  7. JKT Mpwapwa-Dodoma

  8. JKT Makutupora-Dodoma

  9. JKT Mafinga-Iringa

  10. JKT Mlale-Ruvuma

  11. JKT Mgambo-Tanga

  12. JKT Maramba-Tanga

  13. JKT Makuyuni-Arusha

  14. JKT Itaka-Songwe

  15. JKT Lua-Rukwa

  16. JKT Milundikwa-Rukwa

  17. JKT Nachingwea-Lindi

BOFYA HAPA >>NYONGEZA ya vijana waliochaguliwa na maeneo ya makambi ya JKT waliyopangiwa  JKT 2019



waliochaguliwa kujiunga jkt 2019