HESLB - MASWALI NA MAJIBU 21 YA UTARATIBU, SIFA NA VIGEZO VYA UTOAJI MIKOPO KWA 2019/2020
BODI YA MIKOPO (HESLB) TANZANIA
TCU - List Of Universities (Vyuo Vikuu Tanzania) - New Updates
Zipi ni sifa kuu za kupata mkopo wa elimu ya juu?
- Awe mtanzania
- Awe ameomba mkopo kwa utaratibu ulioelekezwa (online)
- Awe amepata udahili (admission) kwenye chuo kinachotambuliwa na jina lake kuwasilishwa Bodi ya Mikopo
- Asiwe na chanzo kingine cha kugharamia masomo yake ya chuo kikuu (mfadhili, ZHELB n.k)
- Maelezo ya kina kuhusu sifa na vigezo hutolewa na Mwongozo
Admission Guide Book 2019/2020 for Form Six Applicants
Admission Guide Book 2019/2020 for Ordinary Diploma/Equivalent Applicants
Ninapaswa kufanya nini ili niweze kuanza kuomba mkopo kwa njia ya mtandao (OLAMS)?
- Soma mwongozo uliotolewa na Bodi ambao unapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz), kisha, fungua mtandao wa maombi (www.olas.heslb.go.tz) ili ujisajili kwa kutumia namba yako ya mtihani wa kidato cha nne na mwaka uliofanya mtihani huo.
Baada ya kujisajili, napaswa kufanya nini?
- Baada ya kujisajili, utapata namba ya kumbukumbu (Control Number) kwenye ‘screen’ ambayo itakuwezesha kufanya malipo ya ada ya maombi ya TZS 30,000/= kwa njia ya benki au simu. Lipa mara moja tu! Kiasi kamili cha TZS 30,000/=
- Baada ya kulipa, utapokea ujumbe (sms) wa uthibitisho wa muamala wako utakaokuwezesha kuendelea na hatua inayofuata ya maombi. Jaza hatua kwa hatua.
Ni nyaraka gani muhimu zinatakiwa wakati wa kuomba mkopo?
Nakala za:- Cheti cha kuzaliwa cha mwombaji kilichothibitishwa na RITA
- Vyeti vya kidato cha IV & VI au Stashahada (Diploma)
- Cheti cha kifo ikiwa umepoteza mzazi kilichothibitishwa na RITA;
- Kitambulisho cha mdhamini (NIDA, Mpiga Kura; Leseni ya Udereva au Pasi ya Kusafiria). Mdhamini anaweza kutumia kimoja kati ya vitambulisho hivi.
- Barua ya taasisi mfadhili (Sponsor) ikiwa ulifadhiliwa katika masomo ya sekondari
- Barua ya Mganga Mkuu wa Wilaya au Mkoa ikiwa mwombaji au mzazi wake ana ulemavu
- Picha (passport size) za mwombaji wa mkopo na mdhamini wake (mdhamini anaweza kuwa mzazi au mlezi)
Je, iwapo nimehitimu kidato cha sita au diploma mwaka huu 2019 na sijapata cheti nitaambatanisha nini?
- Unatakiwa kujaza namba ya mtihani wa kidato cha sita ambayo itaweza kuhakikiwa na mamlaka husika. Kwa mhitimu wa diploma (Stashahada), unaweza kuambatanisha waraka wa matokeo (transcript).
Je, mwanafunzi anaweza kupata usaidizi wa kuomba mkopo kwenye ‘Internet CafĂ©’?
- Ndio. Hata hivyo, unashauriwa kuhakikisha kuwa taarifa zako zimejazwa kwa usahihi. Hakikisha viambatanisho vyote (vyeti, barua n.k) vimewekwa/vimepakiwa kwenye fomu yako mtandaoni.
Je, nikijaza namba yangu ya mtihani isiyokuwa ya NECTA, kwa mfano ya nje ya nchi, nitawezaje kuendelea kuomba mkopo?
- Wakati wa kujisajili, unatakiwa kuchagua kipengele cha ‘Non-NECTA students’ na kujaza kama inavyoelekezwa. Mfumo utakupatia namba ya kidato cha nne tofauti na ile uliyojaza ambayo itatambuliwa na mfumo wa Bodi. Namba hii mpya itatokana na taarifa yako ya namba uliyojazwa awali (isiyokuwa ya NECTA).
Inachukua muda gani fomu kufunguka baada ya kulipa?
- Fomu inafunguka mara tu malipo yanapokamilika. Fomu inapochelewa kidogo kufunguka, mwombaji unashauriwa kutoka (Sign out) na kujaribu kuingia tena (Sign in) katika mtandao ili aweze kuendelea na hatua zinazofuata.
Ikiwa nimelipa lakini sijapokea ujumbe wa kuendelea na maombi, nifanyeje?
- Unatarajiwa kupokea ujumbe mara tu muamala unapokamilika. Ikiwa hautapata ujumbe ndani ya saa moja (dakika 60) baada ya kufanya malipo, unashauriwa kuwasiliana nasi kwa namba ya simu +255 22 550 7910 au 0736 665 533 au barua pepe info@heslb.go.tz
Nitafanyaje ikiwa njia mojawapo ya kulipia mfano, CRDB, NMB, TPB, M-pesa, Airtel Money, Ezy Pesa, Tigo-Pesa, T-Pesa itanigomea kulipa na kuendelea?
- Kwa kuwa kuna njia zaidi ya moja ya kulipia, unashauriwa kutumia njia ya malipo ambayo ni rahisi kwako au inapatikana sehemu uliyopo wakati ukifanya malipo.
Nifanyeje iwapo nimesahau neno langu la siri (Password)?
- Utapaswa kubofya kiunganishi cha “Forgotten the Password?” na kisha utapata neno jipya la siri hapo hapo (kwenye screen) mtandaoni.
Je, ni wapi nitahakiki cheti za kuzaliwa au kifo cha mzazi?
- Vyeti vya kuzaliwa na vya vifo vya wazazi lazima vihakikiwe na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kabla havijapakiwa (uploaded) kwenye mtandao (olams)
Je kuna athari zozote ikiwa nimeambatanisha na kuwasilisha cheti ambacho hakijahakikiwa na RITA au Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar?
- Ndiyo. Maombi yako yatakuwa hayajakamilika na hivyo kutofikiriwa katika hatua ya upangaji mikopo.
- Unapaswa kuhakikisha nyaraka zote (siyo vyeti vya vifo au kuzaliwa tu) zinathibitishwa na mamlaka, taasisi au maafisa waliotajwa katika mwongozo.
Kama simfahamu mzazi wangu, nitajaza nini?
- Unatakiwa kujaza taarifa za mlezi au mtu mwingine anayekulea au kusimamia masuala yako ya Elimu. Ni lazima taarifa za mlezi au msimamizi zithibitishwe na Serikali ya Mtaa unakoishi. Kama mlezi anazo nyaraka rasmi za kukuasili (adoption document) nazo ziambatanishwe.
Je, nikikosea kuchagua ‘Applicant’s Category’ natakiwa kufanya nini?
Ikiwa bado ‘huja-print’, unaweza kurekebisha kwa kurudi kwenye kipengele cha ‘Applicant’s Category’ na kuchagua kipengele sahihi. Iwapo umekamilisha maombi na ku-print fomu yako, unatakiwa kuandika barua ya kuomba kufanyiwa marekebisho, na kuituma HESLB kwa njia ya EMS. Barua hiyo iwe na namba ya kidato cha nne yenye mwaka uliofanya mtihani huo.Kama nina umri wa miaka 30, naweza kuomba mkopo?
- Kwa mwaka wa masomo 2019/2020, umri wa juu wa mwombaji ni miaka 33. Umri umeongezwa ili kuongeza wigo wa wanufaika wa mikopo.
Iwapo niliwahi kupata mkopo zamani na nikaacha, kushindwa au kufukuzwa chuo, nitaweza kupata mkopo mwingine?
- Iwapo uliwahi kuwa mnufaika wa mkopo wa fedha za Serikali, utapaswa kwanza kurejesha mkopo wote au angalau asilimia 25 ya deni lako kabla ya kufikiriwa kupata mkopo mwingine. Deni unalopaswa kulipa utalipata kwenye mtandao (screen) na utatakiwa kulipa kwanza kabla ya kuendelea na maombi ya mkopo mpya.
Kama nina wazazi wasio na uwezo, je niwasilishe uthibitisho wa aina gani ili kupata mkopo?
- Mwombaji ambaye ana mahitaji maalum, ni lazima mahitaji na hali yake ithibitishwe na mamlaka husika kama Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) au taasisi za aina hiyo. Taarifa za aina hii zitapekuliwa kuthibitishwa uhalisia na ukweli wake.
Kama nilikosa mkopo mwaka jana, nikalazimka kuahirisha masomo, natakiwa kuomba tena mkopo mwaka huu?
- Unaruhusiwa kuomba upya mkopo mwaka huu. Maombi yako yatapimwa kwa mwongozo na vigezo vya mwaka 2019/2020. Unashauriwa usome mwongozo kwa makini na kuuzingatia.
- Aidha, kama unasoma mwaka wa pili au wa tatu na kuendelea na una uhitaji wa mkopo, unaruhusiwa kuomba kwa kuzingatia vigezo vya mwaka huu.
Nitafanyaje nisipoweza kumfikia mtoa huduma kwa njia ya Simu zinazoonyeshwa kwenye mtandao?
- Kuna njia mbili za kuwafikia watoa huduma wa kitengo cha usaidizi (Helpdesk) Njia ya kwanza ni kwa simu +255 22 550 7910 au 0736 665 533 na nyingine ni kwa barua pepe info@heslb.go.tz.
- Unashauriwa kuwasilisha taarifa au changamoto husika kwa njia ya barua pepe ili wataalamu waifanyie kazi na kukupigia simu kama itahitajika. Kumbuka kuandika mawasiliano yako ya simu itakayotumika kukupigia.
Je, nitajuaje kama nimejaza fomu ya maombi kwa ukamilifu?
Mwombaji una wajibu wa kuhakikisha nyaraka zote muhimu zimepakiwa kwenye mfumo wa maombi katika nakala laini. Nyaraka hizo ni pamoja na:- Picha ya mwombaji na picha ya mdhamini wako;
- Vivuli vya nakala za vyeti vya kitaaluma zilizothibitishwa na Wakili au Mahakama;
- Vivuli vya nakala za vyeti vya kuzaliwa au kifo zilizothibitishwa na RITA;
- Nakala za barua za ufadhili kutoka katika taasisi zinazotambulika;
- Nakala ya kitambulisho cha mdhamini kilichothibitishwa na Wakili au Mahakama;
- Nakala ya fomu ya maombi iliyosainiwa na kugongwa muhuri na Serikali ya Mtaa, Mahakama au Wakili kama inavyoelekezwa;
- Aidha, nakala halisi ya fomu ya maombi inapaswa kusainiwa na mwombaji na mdhamini wake
- Maelezo ya kina yanapatikana katika mwongozo uliopo kwenye tovuti ya Bodi ya Mikopo (www.heslb.go.tz)
Fomu za maombi ya Mikopo zinawasilishwaje Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu?
Baada ya kuzi-upload na kukamilisha kujaza fomu ya maombi, mwombaji a-print fomu iliyokamilika na kuituma kwenda kwa:Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
Barabara ya Sam Nujoma – Mwenge
S.L.P. 76068
14113 DAR ES SALAAM
Je mwanafunzi anayekwenda kusoma ngazi ya Stashahada (Diploma) anaweza kuomba mkopo?
- Hapana. Wanafunzi wenye sifa za kujiunga na Stashahada hawana sifa za kuomba mkopo kwa mwaka wa masomo 2019/2020.
Mwombaji atajuaje iwapo amepata mkopo?
- Baada ya Bodi kupokea, kuhakiki na kuchambua maombi ya mikopo, majina ya Wanafunzi watakaofanikiwa kupangiwa mikopo yatatangazwa kupitia tovuti ya Bodi ya Mikopo (www.heslb.go.tz) kabla ya kufunguliwa kwa vyuo vya elimu ya juu walikodahiliwa Wanafunzi husika.
Mkopo unatolewa kwenye vipengele (Loanable Items) vipi?
Kulingana na uhitaji, muombaji anaweza kupangiwa mkopo katika moja au baadhi ya vipengele vifuatavyo:- Chakula na malazi
- Ada ya mafunzo
- Vitabu na viandikwa
- Mahitaji maalumu ya kitivo
- Utafiti
- Mafunzo kwa vitendo
Je, utaratibu wa kurejesha mkopo baada ya masomo ni upi?
- Ni wajibu wa kila mnufaika wa mkopo kuhakikisha anarejesha mkopo baada ya kumaliza masomo. Maelezo ya utaratibu yanapatikana katika fomu uliyoombea mkopo. Hakikisha unayasoma kwa makini.
heslb - Bodi ya Mkopo>>Jinsi ya kufanya malipo baada ya kupata control number
Payment Instructions Using Vodacom Mpesa:
- Dial *150*00#
- Select 4. Payments
- Select 5. Government Payment
- Select 1. Control Number
- Enter the Control number (e.g 991120000032)
- Enter Amount (e.g 30,000/=)
- Enter PIN
- Press 1 to Confirm:
Malekezo ya Jinsi ya kulipia kwa Vodacom Mpesa:
- Piga *150*00#
- Chagua 4. LIPA kwa M-Pesa
- Chagua 5. Malipo ya Serikali
- Chagua 1. Number ya Malipo
- Ingiza namba ya malipo (e.g 991120000032)
- Ingiza kiasi (e.g.30,000/=)
- Ingiza namba ya siri.
- Bonyeza 1 kuthibitisha