Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza kufuta matokeo ya mitihani darasa la 7 kwa baadhi ya shule kufuatia kuvuja kwa mitihani wa Taifa.
Share on WhatsAppBiology Lessons & Notes - FORMS I, II, III, IV
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza kuyafuta matokeo ya mitihani ya Darasa la saba kwa shule za msingi zote zilizopo ndani ya Halmashauri ya Chemba, pamoja na baadhi ya shule katika halmashauri ya Kondoa, Kinondoni, Mwanza jiji na Ubungo kwa kosa la kuhusika kwa kuvujisha kwa mitihani ya darasa la saba ikiwa ni kinyume na taratibu na kanuni za mitihani nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Taifa (NECTA) Charles Msonde amesema “Kufuatia kuvunjwa kwa kanuni za mitihani baraza limeamua kufuta matokeo ya kumaliza shule ya msingi ya halmashauri ya Chemba pamoja na shule ya Hazina na Kinondoni, Anyindumina na Font of Joy za Ubungo, Alloiance na New Alliance ya Mwanza jiji pamoja na Kondoa Integrity ya Kondoa Mjini, na watahiniwa wa mtihani hiyo watairudia tena oktoba tarehe 8 na tarehe 9 wiki ijayo." Amesema Charles Msonde.
Aidha baraza hilo limefuta vituo vya mitihani kwa shule nane ambazo zilihusika katika uvujishaji wa mitihani hiyo sambamba na kupendekeza kuondolewa kwenye nafasi za ajira kwa baadhi ya maafisa elimu kata na wilaya waliohusika kwenye udanganyifu huo.