HESLB - HATUA 10 MUHIMU ZA KUZINGATIA - HESLB 2017/2018

ZIFUATAZO NI HATUA 10 MUHIMU ZA KUZINGATIA - HESLB 2017/2018

1. Soma Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa Mwaka 2017-18 kabla ya kufanya lolote.

2. Maombi yatapokelewa kwa njia ya mtandao kuanzia tarehe 6 Agosti – 4 Septemba, 2017;

3. Tembelea tovuti ya Bodi (https://olas.heslb.go.tz) na kujisajili kwa kutumia Namba yako  ya Mtihani wa Kidato cha Nne;

4. Pata Namba ya Kumbukumbu ya Malipo/Reference Number (99117xxxxxxx) baada ya kujisajili ambayo utaitumia kulipa TZS 30,000.00 kwa mkupuo mmoja kwa njia zifuatazo:

• MPesa, AirtelMoney au TigoPesa kwa Namba ya Kampuni 888999. Baada ya kulipa, utatumiwa stakabadhi yako kwa njia ya ‘sms’;

• Tumia Namba ya Kumbukumbu ya Malipo/Reference Number uliyopata kutoka katika mtandao wa OLAMS kufanya malipo katika Tawi lolote au Wakala yeyote wa Benki za CRDB na NMB. Ikiwa una swali, muulize Afisa wa Benki.

5. Fungua mtandao wa OLAMS kwa ajili ya kuendelea na kujaza fomu ya maombi;

6. ‘Print’ fomu uliyokamilisha kujaza kwenye mtandao, ipeleke kwa Kamishna wa Viapo au Wakili/Hakimu na Viongozi wa Serikali ya Mtaa wako kwa ajili ya saini;

7. Thibitisha nakala za vyeti vyote unavyoambatisha na fomu ya maombi kwa Kamishna wa Viapo au Wakili/Hakimu;

8. ‘Upload’ kwenye mtandao (https://olas.heslb.go.tz) kurasa zote zilizosainiwa na kugongwa mihuri pamoja na nakala zote za vyeti zilizothibitishwa na Kamishna wa Viapo au Wakili/Hakimu;

9. Hakikisha unazo nyaraka zifuatazo/zitakazoambatanishwana ombi lako:
i.Fomu ya Maombi iliyosainiwa na Kamishna wa Viapo au Wakili/Hakimu;
ii.Nakala za vyeti vya taaluma zilizothibitishwa na kugongwa muhuri na Kamishna wa Viapo au Wakili/Hakimu;
iii.Nakala ya cheti cha Kuzaliwa kilichothibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA);
iv.Ikiwa ni yatima, nakala ya cheti/vyeti vya vifo vilivyothibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA);
v.Ikiwa ulifadhiliwa, nakala ya barua kutoka taasisi iliyofadhili masomo; na 
vi.Nyaraka nyingine muhimu zinazothibitisha uhitaji wako;

10. Toa nakala (photocopies) za nyaraka zote hapo juu kwa ajili ya kumbukumbu yako. Fomu halisi ya maombi iliyosainiwa na Kamishna wa Viapo au Wakili/Hakimu pamoja na nakala zilizothibitishwa (certified copies) zitumwe kwa njia ya EMS kwenda:

Mkurugenzi Mtendaji, 
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu,  Kitalu Na. 8, Nyumba Na. 45,  Barabara ya Sam Nujoma, Mwenge,  S.L.P. 76068, DAR ES SALAAM.

Hakikisha bahasha inakuwa na fomu ya mwombaji mmoja, anuani ya muombaji ikionyesha namba ya mtihani ya kidato cha nne na mwaka, pamoja na neno “maombi ya mkopo”  


Kusoma mwongozo na vigezo vya utoaji mikopo na ruzuku kwa mwaka wa masomo 2017/2018 bofya hapa>>GUIDELINES AND CRITERIA FOR ISSUANCE OF STUDENTS’ LOANS AND GRANTS FOR THE 2017/2018 ACADEMIC YEAR

HOW TO BECOME A SUCCESSFUL STUDENT

 

Q & A - QUESTIONS AND ANSWERS