MFUMO WA KUTUNUKU MATOKEO YA UPIMAJI/MITIHANI YA TAIFA KWA KUTUMIA JUMLA YA ALAMA (DIVISHENI)

UTARATIBU WA KUTUNUKU MATOKEO YA MITIHANI YA TAIFA - Kidato cha Pili, Kidato cha Nne, Kidato cha Sita.



WHAT DOES IT TAKE TO BECOME A SUCCESSFUL STUDENT?



1.0  UTANGULIZI

Baraza la Mitihani la Tanzania limefanya maboresho ya mfumo wa kutunuku matokeo ya Upimaji na mitihani ya taifa katika ngazi ya elimu ya Sekondari. Maboresho hayo yamefanyika kufuatia maoni ya wadau wa elimu kwa Serikali kuhusu haja ya kuwa na viwango bora vya ufaulu na madaraja yaliyo katika mfumo wa jumla ya alama (Divisheni).

2.0  UTARATIBU WA KUTUNUKU MATOKEO YA MITIHANI YA TAIFA


Uchakataji wa matokeo ya Upimaji wa Kidato cha Pili na mitihani ya Kidato cha Nne na cha Sita utazingatia viwango vya alama , madaraja ya ufaulu na utaratibu wa matumizi ya alama endelevu (CA) kama ifuatavyo:

(a) Viwango vya alama


(i) Kidato cha Pili na cha Nne


GREDIALAMAUZITO WA
GREDI (POINTI)
MAELEZO
A75 -1001Bora sana (Excellent)
B65 -742Vizuri sana (Very Good)
C45 - 643Vizuri (Good)
D30 - 444Inaridhisha (Satisfactory)
F0 - 295Feli (Fail)



DON'T SETTLE INTO A COMFORT ZONE!

 

(ii) Kidato cha Sita


GREDIALAMAUZITO WA
GREDI (POINTI)
MAELEZO
A80 -1001Excelent
B70 -792Very Good
C60 - 693Good
D50 - 594Average
E40 - 495Satisfactory
S35 - 396Subsidiary
F0 -347Fail



BREAST CANCER: Six Steps to Reduce Your Risk of Breast Cancer.

 

(b) Madaraja ya Ufaulu


(i) Madaraja ya Ufaulu yatakuwa katika mfumo wa Jumla ya Alama (Total Point Grading System) au Divisheni. Mtahiniwa aliyefanya masomo yasiyopungua 7 kwa Kidato cha pili na cha Nne na masomo yasiyopungua matatu ya tahasusi (combination) kwa Kidato cha sita atatunukiwa Daraja la I, II, III au IV kwa kufuata wigo wa jumla ya alama (pointi) kama ifuatavyo:

DARAJAFTNA (K2) NA CSEE (K4)ACSEE (K6)MAELEZO
17 - 173 - 9Bora sana (Excellent)
218 - 2110 - 12Vizuri sana (Very Good)
322 - 2513 - 17Vizuri (Good)
426 - 3318 - 19Inaridhisha (Satisfactory)
034 - 3520 - 21Feli (Fail)


(ii) Mtahiniwa aliyefanya idadi ya masomo pungufu ya saba kwa Kidato cha Pili au cha Nne atahesabiwa kuwa amefaulu kwa kiwango cha chini cha ufaulu wa daraja la Nne endapo atafaulu angalau masomo mawili katika Gredii D au somo moja katika Gredi A, B au C.  Aidha,  mtahiniwa wa Kidato cha sita aliyefanya masomo pungufu ya matatu ya tahasusi atatunukiwa ufaulu wa chini wa daraja la Nne endapo atafaulu angalau masomo mawili katika Gredi S au somo moja katika Gredi A, B, C, D na E. 


HOW TO READ AND STUDY TEXTBOOKS

 

(c) Matumizi ya Alama Endelevu (CA)


Uwiano baina ya alama endelevu (CA) na Alama za mtihani wa mwisho (FE) utakuwa ni 30:70. Mchanganuo wa mchango wa alama 30 za CA kwa Kidato cha Nne na cha Sita utakuwa kama ifuatavyo:

CSEE (K4)
Aina ya UpimajiAlama
Upimaji Kidato cha Pili10
Upimaji Kidato cha Tatu (Muhula I, II na Project)10
Mtihani wa Mock Kidato cha Nne10
JUMLA30


ACSEE (K6)
Aina ya UpimajiAlama
Upimaji Kidato  V (Muhula I, II na Project)15
Mtihani wa Mock Kidato cha Sita  15
JUMLA30


3.0 HITIMISHO

Utaratibu wa kutunuku matokeo kwa muundo wa madaraja wa jumla ya alama (Divisheni) ulitumiwa na Baraza la Mitihani la Tanzania kuanzia mwaka 1976 hadi 2013. Hivyo, ni matumaini ya Baraza kuwa mfumo huu utakuwa na tija kwa kuwa unaeleweka vema kwa wadau wa elimu walio wengi.