Majina ya wanafunzi wa kidato cha sita waliochaguliwa kujiunga JKT 2017

Wanafunzi wa kidato cha sita waliochaguliwa kujiunga JKT 2017

Kujiunga jkt 2017

TANGAZO KWA VIJANA WALIOHITIMU KIDATOCHA SITA  WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUZO YA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2017

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu Elimu ya Sekondari Kidato cha Sita kwa mwaka 2017, kutoka Shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria.
 Sanjari na Uchanguzi huo, JKT limewapangia Makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti Makambini kuanzia tarehe 25 – 30 Mei 2017.

Kujiunga jkt 2017
Kujiunga jkt 2017
 Vijana waliochanguliwa, wamepangiwa katika kambi za JKT Rwamkoma – Mara, JKT Msange – Tabora, JKT Ruvu – Pwani, JKT Makutopora – Dodoma, JKT Mafinga – Iringa, JKT Mlale – Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba – Tanga, JKT Makuyuni – Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila – Kigoma.

 Aidha, wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities) wanatakiwa kuripoti kambi ya JKT Ruvu iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.


JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo:

  1. Bukta ya rangi ya ‘Dark blue’ yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu.
  1. Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue.
  1. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari
  1. Soksi ndefu za rangi nyeusi.
  1. Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.
  1. Track suit ya rangi ya kijani au blue.
  1. Nauli ya kwenda makambini na kurudi majumbani.
Mkuu wa JKT anawakaribisha Vijana wote waliochaguliwa ili waweze kujiunga na Vijana wenzao katika kujifunza Uzalendo, Umoja wa Kitaifa, Stadi za kazi, Stadi za maisha na Utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.

Majina ya Wanafunzi Kidato cha Sita Waliochaguliwa Kujiunga JKT 2017


ORODHA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA JKT 2017 NA MAKAMBI WALIYOPANGIWA

 

HOW TO GET READY FOR YOUR EXAMS



Common Job Interview Questions and Answers


Choose When, Where, and How Long To Study