Mahitaji muhimu kwa vijana wanaojiunga JKT 2018 - Form six wanaojiunga JKT 2017 mahitaji muhimu
VIJANA WALIOCHAGULIWA JKT 2018
mahitaji ya jkt
mahitaji jkt 2017
TCU - Change of Procedure for Admissions to Undergraduate Programmes for 2017/2018 Academic year - New Updates
mahitaji ya kujiunga jkt
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu Elimu ya Sekondari Kidato cha Sita kwa mwaka 2017, kutoka Shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria.Sanjari na Uchanguzi huo, JKT limewapangia Makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti Makambini kuanzia tarehe 25 – 30 Mei 2017.
Mahitaji muhimu JKT 2017 |
Aidha, wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities) wanatakiwa kuripoti kambi ya JKT Ruvu iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.
JKT 2017 MAHITAJI MUHIMU
JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo:
Bukta ya rangi ya ‘Dark blue’ yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu.
- Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue.
- Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari
- Soksi ndefu za rangi nyeusi.
- Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.
- Track suit ya rangi ya kijani au blue.
- Nauli ya kwenda makambini na kurudi majumbani.
Mkuu wa JKT anawakaribisha Vijana wote waliochaguliwa ili waweze kujiunga na Vijana wenzao katika kujifunza Uzalendo, Umoja wa Kitaifa, Stadi za kazi, Stadi za maisha na Utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.
JKT T 2017 - BOFYA HAPA KUONA ORODHA YA MAJINA YA VIJANA NA MAKAMBI WALIYOPANGIWA - AWAMU YA KWANZA
JKT T 2017 - BOFYA HAPA KUONA ORODHA YA MAJINA YA VIJANA NA MAKAMBI WALIYOPANGIWA - AWAMU YA PILI
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), linapenda kuutaarifu umma kuwa limeongeza majina ya vijana waliohitimu elimu ya kidato cha sita mwezi Mei 2017 kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria.Vijana hao wanatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa kuanzia tarehe 13 Juni 2017 hadi tarehe 20 Juni 2017.
Mkuu wa JKT, kwa mara nyingine tena, anawakaribisha vijana wote waliochaguliwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.