EDUCATION SYSTEM IN TANZANIA - SERA YA ELIMU TANZANIA
Serikali imekusudia kuleta mapinduzi ya kiuchumi ili kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifkapo mwaka 2025.
Sekta ya elimu na mafunzo, kwa mujibu wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 na Mpango wa muda mrefu wa Maendeleo ya Taifa 2011/12 hadi 2024/25, inatarajiwa kuleta maendeleo
ya haraka ya rasilimaliwatu kwa kutayarisha idadi ya kutosha ya Watanzania walioelimika na kupenda kujielimisha zaidi ili kulifanya Taifa lipate maendeleo na kuwa lenye uchumi wa kati na shindani ifkapo mwaka 2025. Ili kufkia lengo hili, mfumo wa elimu na mafunzo unaotumika nchini lazima utoe fursa za kutosha kwa watu kujielimisha. Hali kadhalika, mfumo huu unawajibika kutoa elimu na mafunzo yenye ubora unaokubalika na kutambulika kitaifa, kikanda na kimataifa. Katika kufanikisha hili, Serikali imekuwa ikitekeleza sera mbalimbali, hususan, Sera ya Elimu na Mafunzo (1995), Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo (1996), Sera ya Taifa ya Elimu ya Juu (1999) na Sera ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa Elimumsingi (2007) na kuwa na mafanikio mbalimbali. Hata hivyo, katika kipindi hicho, changamoto mbalimbali zimejitokeza zikiwemo udhaifu katika mfumo wa elimu na mafunzo, uhaba wa walimu, uhaba wa zana, nyenzo na vifaa na miundombinu ya kufundishia na kujifunzia pamoja na changamoto katika ithibati na uthibiti wa ubora wa shule na vyuo katika ujumla wake vimechangia katika kushuka kwa ubora wa elimu na mafunzo nchini.
BOFIA HAPA KUPAKUA (DOWNLOAD) SERA YA ELIMU