MABADILIKO YA SHULE/TAHASUSI KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI MWAKA 2015
Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM- TAMISEMI) ilitangaza majina ya wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi mwaka 2015, tarehe 30 Juni, 2015. Baada ya majina haya kutangazwa, OWM-TAMISEMI imepokea maombi mengi toka kwa Wazazi/Walezi na Wanafunzi ya kuomba kubadilishiwa Shule na/au Tahasusi kutokana na sababu mbalimbali. OMW-TAMISEMI imeyachambua maombi haya kwa kuzingatia sababu zilizotolewa na waombaji, uwepo wa nafasi kwenye shule walizomba na ufaulu wa mwanafunzi aliyeomba kubadilisha tahasusi.
Kwa wanafunzi ambao majina yao hayajaonekana kwenye orodha hii na wale waliobadilishiwa shule/tahasusi mnahimizwa kwenda kuripoti kwenye shule mlizopangiwa na ikumbukwe kuwa tarehe ya mwisho ya kuripoti ni tarehe 31 Julai, 2015. Kushindwa kufanya hivyo, nafasi zao zitagawiwa kwa wanafunzi waliokosa nafasi.
Imetolewa na
KATIBU MKUU OWM-TAMISEMI
Bofia Hapa: ORODHA YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI MWAKA 2015 WALIOBADILISHIWA SHULE/TAHASUSI
AU
Bofia Hapa: ORODHA YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI MWAKA 2015 WALIOBADILISHIWA SHULE/TAHASUSI