Selform >>kubadili Combination form Five. TAMISEMI Selform
Tamisemi Selform 2021 - Jinsi ya Kubadili Combination kwa wanaotarajia kujiunga na kidato cha tano 2021 (Kubadilisha Combi)
selform - kubadilisha tahasusi (combination) |
KUBADILISHA COMBINATION 2021 (KUBADILISHA SELFORM 2021) - necta huduma za mawasiliano
Jisajili kwanza Hapa ili kubadili combination (Selform) >>TAMISEMI SELFORM 2020 - MIS (Sign Up)
Ikiwa Umeshajisajili Bofya Hapa kubadilisha combination (Selform) >>TAMISEMI - SELFORM - MIS (Sign In)
MUONGOZO WA MWANAFUNZI KATIKA MFUMO WA SELFORM NAMNA YA KUINGIA NA KUBADILISHA MACHAGUO (COMBINATION)
JUKUMU LA MWANAFUNZI KATIKA MFUMO WA SELFORM
- Mwanafunzi (Muhitimu wa Kidato cha Nne (Form Four)) – Jukumu lake kuu katika mfumo wa Selform ni kubadilisha baadhi ya taarifa binafsi kama Home Address, Mobile Number, Email Address na machaguo ya shule, vyuo na tahsusi zake katika seksheni zingine kutokana na ufaulu katika matokeo yake.
1. NAMNA YA KUINGIA KWENYE MFUMO WA SELFORM
- Ukiwa kwenye internet, fungua kivinjari chako (browser mfano, chrome), andika anuani ifuatayo selform.tamisemi.go.tz kupata dirisha la kujaza taarifa zako za kujisajili kama inavyoonekana hapo chini. Bofya Menu ya chini kabisa iliyoandikwa For Candidates, Click here to Register kama mtumiaji ni mara yake ya kwanza.
- Kisha, ujaze taarifa zinazohusika za Index Number kwa format ya Mfano S0101.0020.2018, Jibu swali utakaloulizwa, Jina la Ukoo na Mwaka wa kuzaliwa kama inavyoonekana hapo chini.
- Kisha dirisha litafunguka na kutaka ujaze Password utakayoitumia siku zote. Dirisha lifuatalo litafunguka;
- Ukishaandika Password, mfumo utaonekana katika sura hii kuonesha umefanikiwa kubadili Password;
- Ukishabadili Password, utaitumia kuingia kwa mara nyingine kwa kuandika username mfano S0101.0002.2018 na Password uliyoibadili.
2. PART A: TAARIFA BINAFSI ZA MWANAFUNZI
- Ukishaingia kwenye mfumo, dirisha lifuatalo litafunguka na sehemu zilizozungushiwa tu ndio utaweza kubadili taarifa binafsi. Ukimaliza kujaza bofya Save and Next hapo chini ili kuendelea mbele.
3. PART B1: STUDENT GENERAL CHOICES
- Bofya katika sehemu hii ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo.
4. PART B2: ALTERNATIVE OPTIONS
- Bofya kuingia katika eneo hili ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo ya vyuo vya Kisekta. Ukimaliza bofya SAVE & NEXT.
5. PART C1: FORM V STUDENT DETAILED CHOICES
- Bofya kuingia katika eneo hili ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo ya shule za form V na tahsusi zake: KUMBUKA– Mwanafunzi ataona Possible combinations tu na shule kutokana na ufaulu wa matokeo yake kwa lengo la kubadilisha. Ukimaliza bofya SAVE & NEXT or Save & Go Back.
6. PART C2: TECHNICAL EDUCATION
- Bofya kuingia katika eneo hili ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo ya Vyuo vya Technical na Tahsusi zake: KUMBUKA– Mwanafunzi lazima awe na ufaulu wa Tahsusi ya PCM katika matokeo yake kwa ajili ya kubadilisha eneo hili. Ukimaliza bofya SAVE & NEXT or Save & Go Back.
7. PART C3: HEALTH EDUCATION
- Bofya kuingia katika eneo hili ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo ya Vyuo vyaAfya na Tahsusi zake. Ukimaliza bofya SAVE & NEXT or Save & Go Back.
8. PART C4: DIPLOMA EDUCATION
- Bofya kuingia katika eneo hili ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo ya Vyuo vya Elimu na Tahsusi zake. Ukimaliza bofya SAVE & NEXT or Save & Go Back.
9. PART C5: OTHER COLLEGES
- Bofya kuingia katika eneo hili ili kuendelea kubadilisha taarifa zako za machaguo ya Vyuo Vinginevyo na Tahsusi zake. Ukimaliza bofya SAVE & NEXT or Save & Go Back.