PSLE 2018 EXAM TIMETABLE - TIMETABLE DARASA LA SABA 2018
NECTA PSLE 2019 TIMETABLE.pdf>>RATIBA YA DARASA LA SABA 2019>>PSLE NECTA Results 2019
Standard Seven past papers (PSLE) - NECTA - Past papers za darasa la saba - New Updates
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
RATIBA YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI
PRIMARY SCHOOL LEAVING EXAMINATION TIMETABLE SEPTEMBA 2018
TAREHE NA SIKU | MUDA (SAA) | NAMBA MFICHO | SOMO |
05.09.2018 JUMATANO | 2:00-3:30 | 01 | KISWAHILI |
3:30-4:30 | MAPUMZIKO | ||
4:30-6:30 | 04 04E | HISABATI MATHEMATICS | |
6:30-8:30 | MAPUMZIKO | ||
8:30-10:00 | 02 | ENGLISH LANGUAGE | |
06.09.2018 ALHAMISI | 2:00-3:30 | 05 05E | SAYANSI SCIENCE |
3:30-4:30 | MAPUMZIKO | ||
4:30-6:00 | 03 03E | MAARIFA YA JAMII SOCIAL STUDIES |
TOP 10 SECONDARY SCHOOLS IN TANZANIA 2019 - Shule bora za sokondari.
PSLE 2018 EXAM TIMETABLE - RATIBA DARASA LA SABA 2018
MAELEKEZO MUHIMU- Hakikisha kuwa unayo Ratiba ya Mtihani ya mwaka 2018 iliyoandaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania.
- Kabla ya kufungua bahasha yoyote yenye maswali ya Mtihani, hakikisha kwamba unasoma jina la somo juu ya bahasha husika na kujihakikishia kuwa somo hilo ndilo linalostahili kufanyika wakati huo kulingana na Ratiba ya Mtihani.
- Endapo utata utajitokeza kati ya maelekezo yaliyomo ndani ya Karatasi ya Mtihani na Ratiba ya Mtihani, maelekezo yaliyomo katika karatasi ya Mtihani husika ndiyo yatakayofuatwa.
- Watahiniwa WASIOONA na wale wenye UONI HAFIFU waongezewe MUDA WA ZIADA WA DAKIKA 10 KWA KILA SAA kwa Mtihani wa Kiswahili, English Language, Maarifa ya Jamii na Sayansi.
- Watahiniwa WASIOONA na wale wenye UONI HAFIFU waongezewe MUDA WA ZIADA WA DAKIKA 20 KWA KILA SAA kwa mtihani wa Hisabati.
- Msimamizi wa watahiniwa WASIOONA awe mtaalamu mwaminifu aliye na uwezo wa kusoma maandishi na alama za ‘Braille’.
- Watahiniwa wenye UONI HAFIFU wapewe karatasi za mtihani na za kujibia zenye maandishi yaliyokuzwa, zilizoandaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania kwa matumizi yao.
- Karatasi zenye majibu ya watahiniwa wenye UONI HAFIFU zifungwe kwenye bahasha za pekee. Zisichanganywe na karatasi za watahiniwa wenye Uoni wa kawaida.
- Watahiniwa waelekezwe;
- Kuingia ndani ya chumba cha mtihani nusu saa kabla ya muda wa mtihani na watakaochelewa kwa zaidi ya nusu saa baada ya mtihani kuanza hawataruhusiwa.
- Kufuata maelekezo yote yatakayotolewa na wasimamizi wa mtihani.
- Kuandika namba ya mtihani kwa usahihi.
- Kutofanya mawasiliano ya maneno au kwa njia yoyote baina ya watahiniwa. Ikiwa mtahiniwa ana tatizo anatakiwa kunyosha mkono ili kuomba msaada kwa msimamizi wa mtihani.
- Wakijihusisha katika udanganyifu watafutiwa matokeo yao ya mtihani.