HESLB-ORODHA YA MAJINA WANAOTAKIWA KUSAHIHISHA MAOMBI YA MIKOPO

ORODHA YA MAJINA WANAOTAKIWA KUSAHIHISHA MAOMBI YA MIKOPO 2020/2021

heslb-ORODHA YA MAJINA WANAOTAKIWA KUSAHIHISHA MAOMBI YA MIKOPO

HESLB Orodha ya wanafunzi ambao fomu zao za kuomba mkopo zina Makosa

HESLB - Tunapenda kuwafahamisha waombaji wa mikopo kuwa baada ya kufungwa kwa dirisha la maombi ya mkopo, kazi inayoendelea ni uchambuzi na uhakiki wa maombi hayo na ifikapo Septemba 27, 2020, orodha ya waombaji wanaopaswa kurekebisha maombi yao itawekwa kwenye tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz).
 

HESLB YATOA SIKU TANO (05) ZAIDI KUOMBA MKOPO

Ni kuanzia Oktoba 1 hadi 5, 2020

Lengo ni kuwapa fursa vijana waliokuwa JKT kuomba

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inawajulisha wanafunzi waliomaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) hivi karibuni kuwa mfumo wa kuomba mkopo kwa njia ya mtandao utafunguliwa kwa siku tano (05) kuanzia kesho, Ijumaa, Oktoba 1, 2020 ili kuwawezesha kuomba mkopo.

Uamuzi huu unatokana na maombi ya wanafunzi, wazazi na walezi wa wanafunzi wahitaji ambao hawakuweza kuomba au kukamilisha maombi yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kujiunga na mafunzo katika kambi mbalimbali za JKT kwa mujibu wa sheria.

Aidha, katika muda huo wa siku tano, mfumo pia utakuwa wazi ili kuwawezesha waombaji ambao maombi yao yana upungufu kurekebisha kwa kuweka nyaraka sahihi ili kuiwezesha HESLB kuendelea na hatua nyingine.

“Kwa wanaorekebisha taarifa, wanapaswa kuingia katika akaunti zao walizofungua kuombea mkopo na watapata ujumbe kuhusu maeneo ya kurekebisha. Tunawasihi watumie muda huu wa siku tano kurekebisha na kukamilisha maombi yao ili kutuwezesha kuendelea na hatua inayofuata ili hatimaye wenye sifa wawezeshwe kutimiza ndoto zao,” amesema Mkurugenzai Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru.

Katika mwaka wa masomo 2020/2021, Serikali imetenga TZS Bilioni 464 zitakazowanufaisha jumla ya wanafunzi 145,000. Kati yao, wanafunzi 54,000 watakuwa wa mwaka wa kwanza na wengine 91,000 ni wanafunzi wanufaika wanaoendelea na masomo. Mwaka 2019/2020 jumla ya TZS 450 bilioni zilitengwa na zimewanufaisha jumla ya wanafunzi 132,119. 

MAJINA YA WALIOPATA MKOPO

ORODHA YA MAJINA WANAOTAKIWA KUSAHIHISHA MAOMBI YA MIKOPO 2019/2020

HESLB imetoa orodha ya waombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2019/2020 ambao fomu zao zina upungufu ili wafanye marekebisho kwa siku nne kuanzia kesho Jumatatu tarehe 30 Septemba 2019 ambapo pia mwongozo wa jinsi ya kufanya marekebisho utatolewa..

Hatua ya HESLB inafuatia kukamilika kwa uhakiki wa maombi ya mikopo ambapo imebainika baadhi ya fomu za maombi ya mikopo zina upungufu unaozuia kuendelea na hatua ya kupangiwa mikopo.

Upungufu huo ni pamoja na kukosa nyaraka ama viambatanisho vilivyothibitishwa na mamlaka husika na saini za waombaji na wadhamini wao.
  • Ili kuona orodha ya majina na marekebisho yanayohitajika kwa Shahada ya kwanza *bofya hapa.*

  • Ili kuona orodha ya majina na marekebisho yanayohitajika kwa Shule ya Sheria (Law School of Tanzania) *bofya hapa.*

  • Ili kuona orodha ya majina na marekebisho yanayohitajika kwa Shahada za Uzamili na Uzamivu*bofya hapa.*


majina ya waliokosea kuomba mkopo 2020/2021