HESLB - ORODHA YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO

HESLB - Orodha ya majina ya wanafunzi waliopata mkopo 2020/2021, heslb - awamu ya kwanza ya majina ya waliopata mikopo 2020/2021, HESLB Bodi ya mikopo first batch 2020/21

  Share on WhatsApp

HESLB - ORODHA YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO

HESLB  LOAN BENEFICIARIES

Loan Beneficiaries November 2020 - Majina ya Waliopata Mkopo 2020/2021


HESLB - ORODHA YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO 2020/2021(yemetangazwa leo 11/11/2020 tunasubiri orodha ya majina kwenye PDF) AU Ingia kwenye Account Yako hapa uangalie kama umepata mkopo (Loan Status) >> Online Loan Application and Management System



Taarifa rasmi kuhusu HESLB, zikiwemo zinazohusu wanafunzi wanaopangiwa mkopo zitatolewa kuanzia Novemba 10, 2020 kupitia akauntiwalizotumia kuomba mkopo (SIPA – Student’s Individual PermanentAccount).

Taarifa pia zitatolewa kupitia vyombo vya habari, tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz) na mitandao ya kijamii ya HESLB ambayo ni twitter, instagram na facebook kwa jina la ‘HESLB Tanzania’.

List of loan beneficiaries 2020/2021 - majina ya waliopata mkopo 2020/2021

HESLB - Tunapenda kuwafahamisha waombaji wa mikopo kuwa baada ya kufungwa kwa dirisha leo Alhamisi (Septemba 10, 2020) saa 6:00 usiku , kazi inayoendelea ni uchambuzi na uhakiki wa maombi hayo na ifikapo Septemba 27, 2020, orodha ya waombaji wanaopaswa kurekebisha maombi yao itawekwa kwenye tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz). 

Orodha ya majina ya wanafunzi waliopata mkopo kwa mwaka wa 2019/2020


Wanafunzi 30,675 waliopata mikopo awamu ya kwanza

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha ya awamu ya kwanza yenye wanafunzi 30,675 wa Mwaka wa Kwanza kwa mwaka wa masomo 2019/2020 waliofanikiwa kupata mikopo yenye thamani ya TZS 113.5 bilioni.

Katika mwaka huu wa masomo, Serikali imetenga TZS 450 bilioni zinazolenga kuwanufaisha jumla ya wanafunzi 128,285. Kati yao, zaidi ya wanafunzi 45,000 ni wa mwaka wa kwanza na wengine 83,285 ni wenye mikopo wanaoendelea na masomo. Mwaka 2018/2019, fedha zilizotengwa na kutolewa zilikua TZS 427.5 bilioni na ziliwanufaisha jumla ya wanafunzi 123,283 wakiwemo 41,285 wa mwaka wa kwanza.

Akizungumza na wanahabari leo (Alhamisi, Oktoba 17, 2019) na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru, amesema katika orodha hiyo, wanaume ni 19,632 (64%) na wanawake ni 11,043 (36%).

Badru amefafanua kuwa waombaji mikopo wafunfue akaunti zao binafsi (SIPA – Student’s Individual Permanent Account) walizofungua kuomba mkopo kupitia mfumo wa HESLB (olas.heslb.go.tz) ili kupata taarifa za mikopo. KUONA ORODHA YA AWAMU YA KWANZA, BOFYA HAPA.AU 

HESLB - ORODHA YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO


                                                            Makundi Maalum – Yatima, Wenye ulemavu n.k

Kuhusu makundi maalum yenye uhitaji, Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema katika orodha ya awamu ya kwanza yenye wanafunzi 30,675, wapo wanafunzi 6,142 ambao ni yatima au wamepoteza mzazi mmoja, wenye ulemavu 280 na wengine 277 wanaotoka katika kaya zinazofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

“Katika makundi maalum pia tuna wanafunzi 1,890, sawa na asilimia 6 ya wanafunzi 30,675 wa awamu ya kwanza ambao walisoma shule binafsi lakini kutokana na hali duni ya uchumi, walifadhiliwa na walithibitisha kwa kuweka nyaraka sahihi,” amesema Badru.

                                                               Kutangazwa orodha ya awamu ya pili

Kuhusu awamu ya pili, Badru amesema HESLB kabla ya Oktoba 25 ya wiki ijayo baada ya kukamilishwa kwa uchambuzi wa maombi ya mikopo kutoka kwa wanafunzi waliochelewa kukamilisha taratibu za udahili au kuchelewa kurekebisha maombi yao ya mkopo mtandaoni.

                                                                               Wito kwa wanafunzi

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Uchambuzi na Upangaji Mikopo wa HESLB Dr. Veronica Nyahende amewataka wanafunzi ambao taarifa zao hazijakamilika, kukamilisha ili wenye sifa wapangiwe mkopo.

“Kuna kama wanafunzi 1,000 ambao maombi yao hayajakamilika, watumie muda huu hadi tarehe 19 kukamilisha ili wenye sifa nao tuwapangie mkopo,” amesema. 

majina ya waliopata mkopo 2020/21

MTIHANI WA TAIFA DARASA LA SABA MASWALI NA MAJIBU - PSLE NECTA EXAMS QUESTIONS &; ANSWERS


MATOKEO YA DARASA LA SABA 2020 . NECTA PSLE RESULTS 2020