UTHIBITISHO - MAELEKEZO MAHSUSI KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA ELIMU YA UFUNDI MWAKA 2020
Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Ufundi:
Wanafunzi waliopangwa kwenye Vyuo vya Elimu ya Ufundi vilivyopo chini ya NACTE wanatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:
- Kuthibitishakukubali kujiunga na kozi zinazosimamiwa na Baraza Ia Taifa Ia Elimu ya Ufundi (NACTE) baada ya siku saba (7) kuanzia siku ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi hadi tarehe 15 Agosti, 2020.
- Mwanafunzi atafanya uthibitisho kupitia kiunganishi kinachoitwa UthibitishoTAMISEMI katika tovuti ya Baraza Ia Taifa Ia Elimu ya Ufundi (NACTE) ambayo ni www.nacte.go.tz i|i kukubali kuchaguliwa kwenye kozi na chuo alichopangiwa.
- Wanafunzi ambao hawatathibitisha kukubali nafasi walizochaguliwa, nafasi zao zitachukuliwa na wanafunzi wengine wanaoendelea kuomba katika Vyuo hivyo kwa njia ya mtandao.
- Wanafunzi wanaotaka kufanya mabadiliko ya kozi au chuo walichochaguliwa wanaruhusiwa kufanya hivyo kuanzia tarehe 01 Agosti hadi 30 Agosti, 2020 kupitia mtandao wa NACTE.
- Vyuo ambavyo vimepangiwa wanafunzi vitapata orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kutoka NACTE kwa njia ya Mfumo (kupitia Institution Panel) baada ya muda wa kuthibitisha na kuhama kukamilika.
- Maelekezo ya namna ya kuwasajili wanafunzi watakaoripoti Vyuoni kuanza masomo yatatolewa na Baraza Ia Taifa Ia Elimu ya Ufundi (NACTE)
- Wanafunzi waliopangwa katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kwa masomo ya cheti na stashahada hawatahusika na utaratibu wa NACTE wa kubadilisha kozi na vyuo, hivyo wanapaswa kuwasiliana na vyuo husika.
Form Six Necta Past Papers - for Revision - New Updates
Wanafunzi wote wa bweni waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka, 2020 wanatakiwa kuripoti shuleni tarehe 18 Julai, 2020 tayari kuanza masomo tarehe 20 Julai 2020. Aidha, wanafunzi wa kutwa waripoti na kuanza masomo tarehe 20 Julai 2020. Wanafunzi ambao hawataripoti ndani ya wiki mbili tangu tarehe ya kufungua shule nafasi zao zitachukuliwa na wanafunzi wengine ambao hawakupangiwa shulekatika awamu hii.
Uhamisho wa shule utaruhusiwa baada ya kukamilika kwa Muhula wa Kwanza wa masomo, na zoezi hilo litafanyika kwa kuzingatia uwepo wa nafasi kwenye Shule kwa idhini ya Maafisa Elimu wa Mikoa husika. Hivyo, hakutakuwa na fursa ya kufanya mabadiliko yoyote ya shule kwa sasa ngazi ya Mikoa, Halmashauri na Shule.