TCU Tanzania - Kufunguliwa Dirisha la Udahili

TCU - KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA UDAHILI WA SHAHADA YA KWANZA, MWAKA WA MASOMO 2020/2021

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inapenda kufahamisha umma, Taasisi za Elimu ya Juu na Wadau wote rva Elimu ya juu ndani na nje ya nchi kuwa kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya Kidato cha Sita, Tunne imefungua dirisha la kwanza la maombi ya udahili wa Shahada ya Kwanza kuanzia leo tarehe 26/812020 badala ya tarehe 31/8/2020 iliyokuwa imepangwa hapo awali. Dirisha hili litakuwa wazi hadi tarehe 25 Septemba, 2020.

Tume inaendelea kuwahimiza waombaji wote wa udahili kuendelea kupata taarifa rasmi kupitia tovuti ya TGU www.tcu.qo.tz , tovuti za vyuo vilivyoruhusiwa kudahili wanafunzi wa Shahada za Kwanza, pamoja na taarifa mbalimbali zinazotolewa na TCU kupitia vyombo vya habari. Vile vile Tume inawahimiza waombaji wa udahili na wananchi kwa ujumla kuhudhuria Maonesho ya 15 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yatakayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam ambapo watapata fursa  ya kuonana ana kwa ana na Vyuo vya Elimu ya  Juu. Maonesho hayo yatafanyika kuanzia tarehe 31 Agosti hadi 5 Septemba, 2020.
 
 Ili kufahamu sifa stahiki kwa makundi matatu yaliyotajwa hapo juu, waombaji wanaelekezwa kusoma vigezo vilivyooneshwa katika kitabu cha mwongozo cha TCU (Undergraduate Admission Guidebook for 2020/2021