Tamisemi kubadili chuo - kubadili kozi

TAMISEMI - KUBADILI CHUO AU KOZI KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA NA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (OR-TAMISEMI) KWA MWAKA WA MASOMO 2020/2021


Share on WhatsApp 


TAMISEMI - KUBADILI CHUO AU KOZI KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA NA OR-TAMISEMI KWA MWAKA WA MASOMO 2020/2021 


Mpaka 27 Julai, 2020 wanafunzi 28,668 wamethibitisha kati ya 45,593 waliopangiwa kozi mbalimbali katika vyuo vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi. Hata hivyo, jumla ya wanafunzi 16,925 hawajathibitisha nafasi hizo mpaka sasa.

 Aidha, Baraza, linapenda  kuwafahamisha wanafunzi wote waliochaguliwa na OR-TAMISEMI kwamba:
  1. Wanapaswa wathibitishe kuchaguliwa kwao hata kama wanahitaji kubadili kozi au vyuo walivyopangiwa;
  2. Hakuna mwanafunzi atakayeweza kubadili kozi au chuo kama hatakuwa amethibitisha kupitia tovuti ya NACTE;
  3. (Uhamisho/kubadili chuo au kozi kunamanisha kujaza nafasi zilizowazi kutokana na kutothibitisha; na
  4. Waombaji ambao hawajathibitisha hadi tarehe 15 Agosti, 2020 watapoteza nafasi zao walizochaguliwa na OR-TAMISEMI.

Hivyo, Baraza linawafahamisha waombaji kuwa zoezi la kuomba kubadilisha kozi au kuhama chuo litaanza tarehe 16  hadi 31 Agosti, 2020.

Baraza linawashauri wanafunzi waliopangiwa vyuo kuthibitisha kupitia tovuti ya Baraza (www.nacte.go.tz) kabla ya tarehe 15/08/2020 kama ilivyopangwa hapo awali. Baada ya tarehe hiyo hakutokuwa na nafasi nyengine ya kuthibitisha.