RATIBA YA MTIHANI WA DARASA LA NNE 2019
RATIBA YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (STANDARD FOUR NATIONAL ASSESSMENT TIMETABLE) NOVEMBA, 2019
SFNA TIMETABLE 2019
TAREHE NA SIKU
|
MUDA (SAA)
|
NAMBA MFICHO
|
SOMO
|
20.11.2019 JUMATANO |
2:00-3:30 | 06 06E |
URAIA NA MAADILI CIVIC AND MORAL EDUCATION |
3:30-4:30 | MAPUMZIKO | ||
4:30-6:00 | 04 04E |
HISABATI MATHEMATICS |
|
6:00-8:00 | MAPUMZIKO | ||
8:00-9:30 | 01 | KISWAHILI | |
|
|
|
|
21.11.2019 ALHAMISI |
4:30-6:00 | 05 05E |
SAYANSI NA TEKNOLOJIA SCIENCE AND TECHNOLOGY |
6:00-8:00 | MAPUMZIKO | ||
8:00-9:30 | 03 03E |
MAARIFA YA JAMII SOCIAL STUDIES |
PATA MATOKEO YA DARASA LA nne 2018/2019 (SHULE ZA MSINGI) KIMKOA
MAELEKEZO MUHIMU- Hakikisha kuwa unayo Ratiba ya Upimaji wa mwaka 2019 iliyoandaliwa na Baraza laMitihani la Tanzania.
- Kabla ya kufungua bahasha yoyote yenye maswali ya upimaji, hakikisha kwambaunasoma jina la somo juu ya bahasha husika na kujihakikishia kuwa somo hilo ndilo linalostahili kufanyika wakati huo kulingana na Ratiba ya Upimaji.
- Endapo utata utajitokeza kati ya maelekezo yaliyomo ndani ya Karatasi ya Upimaji na Ratiba ya Upimaji, maelekezo yaliyomo katika karatasi ya upimaji husika ndiyo yatakayofuatwa.
- Wanafunzi WASIOONA na wale wenye UONI HAFIFU waongezewe MUDA WA ZIADA WA DAKIKA 10 KWA KILA SAA kwa upimaji wote isipokuwa DAKIKA 20 KWA KILA SAA kwa somo la Hisabati.
- Msimamizi wa Wanafunzi WASIOONA awe mtaalamu mwaminifu aliye na uwezo wa kusoma maandishi na alama za ‘Braille’.
- Wanafunzi wenye UONI HAFIFU wapewe karatasi za upimaji na za kujibia zenye maandishi yaliyokuzwa, zilizoandaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania kwa matumizi yao.
- Wanafunzi waelekezwe;
- Kuingia ndani ya chumba cha upimaji nusu saa kabla ya muda wa upimaji na watakaochelewa kwa zaidi ya nusu saa baada ya upimaji kuanza hawataruhusiwa.
- Kufuata maelekezo yote yatakayotolewa na wasimamizi wa upimaji.
- Kuandika jina kamili na namba ya upimaji kwa usahihi.
- Kutofanya mawasiliano ya maneno au kwa njia yoyote baina yao. Ikiwa mwanafunzi ana tatizo anatakiwa kunyoosha mkono ili kuomba msaada kwa msimamizi wa upimaji.
- Wakijihusisha au wakifanya udanganyifu watafutiwa matokeo yao ya upimaji.