Ajira za ualimu Tamisemi>>ajira ya walimu 2020
NAFASI ZA AJIRA ZA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI. AJIRA ZA UALIMU
Ajiara za ualimu Tamisemi - OR-TAMISEMI inawatangazia walimu wenye sifa kutuma maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha ajira.tamisemi.go.tz - OnlineTeacher Employment Application System – OTEAS.
Walimu wanaotakiwa kutuma maombi ni wenye sifa za kitaaluma kama ifuatavyo:
A. WALIMU WATAKAOAJIRIWA SHULE ZA MSINGI
- Mwalimu Daraja la IIIA - mwenye Astashahada (Cheti) ya Ualimu;
- Mwalimu Daraja la IIIB - mwenye Stashahada (Diploma ya Ualimu katika masomo ya English, Civics, Historia, Jiografia na Kiswahili;
B. WALIMU WATAKAOAJIRIWA SHULE ZA SEKONDARI
- Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Shahada ya Ualimu waliosomea Elimu Maalum;
- Mwalimu Daraja la IIIB - mwenye Stashahada (Diploma) ya Ualimu waliosomea Elimu Maalum;
- Mwalimu Daraja la IIIB - mwenye Stashahada ya Ualimu somo la Physics, Mathematics , Biology & Chemistry;
- Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Shahada ya Ualimu somo la Agriculture Science;
- Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Shahada ya Ualimu somo la Home Economics;
- Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Shahada ya Ualimu somo la Physics, Mathematics, Chemistry & Biology;
- Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Shahada ya Ualimu somo la Book Keeping, Commerce, Accounts & Economics; na
- Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Shahada ya Ualimu somo la English, Civics & General Studies.
- Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Mahitaji Maalum aliyehitimu Shahada ya Ualimu kwa masomo ya English, Civics, General Studies, History, Geography & Kiswahili.
- Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Shahada ya Ualimu kwa masomo ya English, Civics, General Studies, History, Geography & Kiswahili.
C. SIFA ZA JUMLA
Waombaji wa nafasi tajwa hapo juu wawe na sifa za jumla zifuatazo:-- Awe ni Mtanzania;
- Awe amehitimu chuo kinachotambulika na Serikali kati ya mwaka 2014 hadi 2017; isipokuwa kwa wahitimu wa Elimu ya Ualimu wa masomo ya Fizikia na Hisabati;
- Asiwe na umri wa zaidi ya miaka arobaini na tano (45) wakati wa kutuma maombi haya;
- Walimu waliowahi kutuma maombi na hawajaajiriwa wanapaswa kutuma maombi upya.