waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2018 - Tarehe ya kuanza masomo

JAMJ-IURI YA MUUNGANO WA TANZANIA  OFISI YA RAIS - T AMISEMI



TAARIFA KWA UMMA 

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2018 wataanza muhula wa kwanza tarehe 16 Julai, 2018. Wanafunzi wote wanapaswa kuripoti katika Shule aliyopangiwa kwa muda uliopangwa. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya mwisho ya kuripoti, nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi. 


Mwanafunzi aliyechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, anapaswa kupakua (Dowuload) fomu ya kujiunga na shule husika kwenye mtandao. Mwanafunzi hapaswi kwenda kuchukua fomu ya kujiunga katika shule aliyopangwa na haruhusiwi kupiga simu. Aidha,

wanafunzi waliopangwa kwenye Vyuo vya Elimu ya Kati inabidi kufanya UTHIBffiSHO kuanzia tarehe 17 Juni, 2018 hadi ifikapo tarehe 8 Agosti, 2018 wa kukubali kujiunga na Kozi na Vyuo walivyopangiwa kwa njia ya mtandao. Uthibitisho huo utafanyika kupitia tovuti ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ya www.nacte.go.tz katika kiunganishi kinachoitwa Uthibitisho TAMISEMI.
 
Mwanafunzi atakayeshindwa kuthibitisha kozi na chuo alichopangiwa, nafasi yake itachukuliwa na wanafunzi wengine. Mwanafunzi atakayetaka kufanya mabadiliko ya kozi na chuo alichopangiwa ataruhusiwa kufanya hivyo kuanzia tarehe 9 Agosti, 2018 hadi 23 Agosti, 2018 kupitia tovuti ya NACTE ya www.nacte.go.tz. 


Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, Vyuo vya Ufundi na Vyuo vya Kati vinavyosimamiwa na NACTE kwa mwaka 2018 pamoja na fomu za kujiunga na shule joining instructions) inapatikana kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais - T AMISEMl ya www.tamisemi.go.tz na Baraza la Taiia la Elimu ya Ufundi {NACTE) ya www .nacte.go.tz


Source:-
Imetolewa na Katibu Mkuu,
OR-TAMISEMI