Form one selection - Mkoa wa Dar es salaam Tanzania

Form one selection Mkoa wa Dar Es Salaam 2020/2021


form one selection mkoa wa dar es salaam

UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA, 2021

CHAGUA HALMASHAURI

MTIHANI WA TAIFA KIDATO CHA NNE MASWALI NA MAJIBU - FORM FOUR PAST PAPERS QUESTIONS AND ANSWERS

 Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2020 Shule za Sekondari za Serikali

ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2020 - Mkoa wa Dar es salaam - New Updates


WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2019 - Mkoa wa Dar es salaam

SELECTION ILALA 2019.pdf


SELECTION KINONDONI 2019.pdf


SELECTION UBUNGO 2019.pdf


SELECTION KIGAMBONI 2019.pdf


SELECTION TEMEKE 2019.pdf



MKOA WA DAR ES SALAAM - TAARIFA KUHUSU UCHAGUZI WA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2019 KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM

Mkoa wa Dar es Salaam ulikuwa na jumla ya wanafunzi 70,948 waliosajiliwa kufanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi mwaka huu 2018. Kati yao wavulana ni 33,989 na wasichana ni 36,959. Idadi ya watahiniwa waliofanya mtihani huo ni 70,303 sawa na asilimia 99.091, kati yao wavulana ni 33,623 na wasichana ni 36,680.  Watahiniwa 645 sawa na asilimia 0.909 ikiwa wavulana 367 na wasichana 278 hawakufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utoro wanafunzi 545, vifo 11, ugonjwa 17 na sababu zingine 72.

Watahiniwa 64,861 (Wavulana 31,234 na wasichana 33,627) sawa na asilimia 92.261 wamefaulu mtihani huo. Ufaulu huo umepanda kutoka asilimia 87.82 ya mwaka 2017 hadi asilimia 92.261 kwa mwaka 2018 sawa na ongezeko la asilimia 4.441.  Matokeo hayo yameufanya Mkoa wa Dar es Salaam kuwa katika nafasi ya kwanza (01) Kitaifa kati ya Mikoa 26. Aidha, wanafunzi wote 64,861 waliofaulu sawa na 100% wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2019.

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na shule za ufaulu mzuri zaidi ni 68 wavulana 37 na wasichana 31, Shule za Bweni Ufundi 77 wavulana ni 70 na wasichana 7 na Shule za Bweni kawaida 24, wavulana 12 na wasichana 12.  Katika Shule za Mkoa zinazochukua wanafunzi wa Mkoa wa Dar es Salaam jumla ya wanafunzi 1,810 wamechaguliwa, ambapo  wavulana ni 840 na wasichana 970.  Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga katika Shule za Sekondari za Serikali za Wananchi ni 62,635 wakiwemo wavulana 30,153 na wasichana 32,482. Wanafunzi wenye mahitaji maalum waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza ni 247 (wavulana 122 na wasichana 125).

Kwa mchanganuo Kimanispaa, waliochaguliwa kwa Manispaa ya Ilala ni 21,400, Kigamboni 3,180, Kinondoni 11,940, Temeke 17,183 na Ubungo ni 11,158.


Kuhusu asilimia ya wanafunzi ya kujiungana Shule za Sekondari kwa waliofanya mtihani (transition rate) kwa Mkoa ni asilimia 92.259.  Katika Manispaa ya Ilala (Mjini) ni asilimia 95.592, Ilala (Vijijini) asilimia 90.501, Kinondoni 95.696, Temeke 90.247, Kigamboni 92.227 na Ubungo 89.788.  Hivyo idadi kubwa zaidi ya wanafunzi waliomaliza Darasa la Saba wamepata nafasi za kujiunga na Shule za Sekondari Manispaa ya Kinondoni ikifuatiwa na Ilala Mjini, Kigamboni, Ilala Vijijini, Temeke na Ubungo.   Hakuna nafasi wazi zilizobaki kwa Manispaa zote.

Kwa namna ya pekee, napenda kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa jitihada inazozifanya kuhakikisha Mpango wa upatikanaji wa Elimumsingi bila Malipo unatekelezwa kama ulivyokusudiwa.  Nawashukuru pia Maafisa Elimu, Walimu, Wajumbe wa Kamati za Shule katika Manispaa zote  na Wadau mbalimbali kwa juhudi za usimamizi na uboreshaji wa utoaji wa elimu, pamoja na wazazi na walezi wote kwa malezi na ufuatiliaji wa watoto wao.


Nachukua fursa hii kuwataka wazazi na walezi wa wanafunzi hawa kuwapeleka watoto wao kwenye shule walizopangiwa tarehe 7/01/2019 bila kukosa.  Aidha, ninawakumbusha Wakuu wa Shule 147 ambazo 50 (Manispaa ya Ilala), 14 (Kigamboni), 25 (Kinondoni), 29 (Temeke) na 29 (Ubungo)  zinazopokea wanafunzi wa Kidato cha Kwanza Mkoani Dar es Salaam kuzingatia Waraka wa Elimu Namba 3 wa mwaka 2016 kuhusu utekelezaji wa Elimumsingi bila Malipo.


Nazishukuru Kamati za Uendeshaji wa Mitihani za Wilaya na Mkoa, Sekretarieti ya Uchaguzi wa Wanafunzi ya Mkoa kwa kufanya kazi hii kwa umakini na uadilifu mkubwa, lakini pia Kamati ya Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza ya Mkoa kwa kukamilisha kazi hii muhimu kwa muda na kwa ufanisi.  Orodha ya Majina ya wanafunzi waliochaguliwa inapatikana kwa kila Mratibu Elimu Kata, Mbao za Matangazo za kila Halmashauri na Website ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambayo ni www.dsm.go.tz.



Abubakar M. Kunenge
KATIBU TAWALA MKOA
DAR ES SALAAM



UTANGULIZI FINAL 2018.pdf