RATIBA YA MTIHANI WA DARASA LA NNE 2018 - SFNA NECTA TIMETABLE 2018

SFNA TIMETABLE 2018 - RATIBA YA DARASA LA NNE 2018

RATIBA YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (STANDARD FOUR NATIONAL ASSESSMENT TIMETABLE) NOVEMBA, 2018

SFNA TIMETABLE 2018

TAREHE NA SIKU  MUDA (SAA) NAMBA MFICHO     SOMO
22.11.2018
ALHAMISI 
2:00-3:30   01  KISWAHILI 
3:30-4:30 
MAPUMZIKO
4:30-6:00  04 
04E
HISABATI
MATHEMATICS 
6:00-8:00 
MAPUMZIKO 
8:00-9:30 03
03E
MAARIFA YA JAMII
SOCIAL STUDIES




23.11.2018
IJUMAA 
2:00-3:30   05
05E 
SAYANSI NA TEKNOLOJIA
SCIENCE AND TECHNOLOGY 
3:30-4:30 
MAPUMZIKO
4:30-6:00  02  ENGLISH LANGUAGE
6:00-8:00
MAPUMZIKO 
8:00-9:30 06
06E
URAIA NA MAADILI
CIVIC  AND MORAL EDUCATION

PATA MATOKEO YA DARASA LA nne 2018/2019 (SHULE ZA MSINGI) KIMKOA

RATIBA DARASA LA NNE 2018

MAELEKEZO MUHIMU
  1.  Hakikisha kuwa unayo Ratiba ya Upimaji wa mwaka 2018 iliyoandaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania. 
  2. Kabla ya kufungua bahasha yoyote yenye maswali ya upimaji,  hakikisha kwamba unasoma jina la somo juu ya bahasha husika na kujihakikishia kuwa somo hilo ndilo linalostahili kufanyika wakati huo kulingana na Ratiba ya Upimaji.
  3. Endapo utata utajitokeza kati ya maelekezo yaliyomo ndani ya Karatasi ya Upimaji na Ratiba ya Upimaji, maelekezo yaliyomo katika karatasi ya upimaji husika ndiyo yatakayofuatwa.
  4. Wanafunzi WASIOONA na wale wenye UONI HAFIFU waongezewe MUDA WA ZIADA WA DAKIKA 10 KWA KILA SAA kwa upimaji wote isipokuwa  DAKIKA 20 KWA KILA SAA  kwa somo la Hisabati.
  5. Msimamizi wa Wanafunzi WASIOONA awe mtaalamu mwaminifu aliye na uwezo wa kusoma maandishi na alama za ‘Braille’.
  6. Wanafunzi wenye UONI HAFIFU wapewe karatasi za upimaji na za kujibia zenye maandishi yaliyokuzwa, zilizoandaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania kwa matumizi yao.
  7. Karatasi zenye majibu ya Wanafunzi wenye UONI HAFIFU zifungwe kwenye bahasha za pekee. Zisichanganywe na karatasi za Wanafunzi wenye Uoni wa kawaida. 
  8. Wanafunzi waelekezwe;
  • Kuingia ndani ya chumba cha upimaji nusu saa kabla ya muda  wa upimaji na watakaochelewa kwa zaidi ya nusu saa baada ya upimaji kuanza hawataruhusiwa.
  • Kufuata maelekezo yote yatakayotolewa na wasimamizi wa upimaji.
  • Kuandika jina kamili na namba ya upimaji kwa usahihi.
  • Kutofanya mawasiliano ya maneno au kwa njia yoyote baina yao. Ikiwa mwanafunzi ana tatizo anatakiwa kunyoosha mkono ili kuomba msaada kwa msimamizi wa upimaji.
  • Wakijihusisha au wakifanya udanganyifu watafutiwa matokeo yao ya upimaji.