ELIMU TANZANIA - SERA YA ELIMU NA MAFUNZO

EDUCATION SYSTEM IN TANZANIA -  SERA YA ELIMU TANZANIA



Serikali imekusudia kuleta mapinduzi ya kiuchumi ili kuibadili Tanzania  kuwa  nchi  ya  uchumi  wa  kati  ifkapo  mwaka  2025.

 Sekta ya elimu na mafunzo, kwa mujibu wa Dira ya Maendeleo ya  Taifa  ya  2025  na  Mpango  wa  muda  mrefu  wa  Maendeleo ya  Taifa  2011/12  hadi  2024/25,  inatarajiwa  kuleta  maendeleo
 ya haraka ya rasilimaliwatu kwa kutayarisha idadi ya kutosha ya Watanzania walioelimika na kupenda kujielimisha zaidi ili kulifanya Taifa lipate maendeleo na kuwa lenye uchumi wa kati na shindani ifkapo mwaka 2025. Ili kufkia lengo hili, mfumo wa elimu na mafunzo unaotumika nchini lazima utoe fursa za kutosha  kwa  watu  kujielimisha.  Hali  kadhalika,  mfumo  huu unawajibika kutoa elimu na mafunzo yenye ubora unaokubalika na kutambulika kitaifa, kikanda na kimataifa. Katika kufanikisha hili,  Serikali  imekuwa  ikitekeleza  sera  mbalimbali,  hususan, Sera ya Elimu na Mafunzo (1995), Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo (1996), Sera ya Taifa ya Elimu ya Juu (1999) na Sera ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa Elimumsingi (2007) na kuwa na mafanikio mbalimbali. Hata hivyo, katika kipindi hicho, changamoto mbalimbali zimejitokeza zikiwemo udhaifu katika mfumo wa elimu na mafunzo, uhaba wa walimu, uhaba wa zana, nyenzo na vifaa na miundombinu ya kufundishia na kujifunzia  pamoja  na  changamoto  katika  ithibati  na  uthibiti wa ubora wa shule na vyuo katika ujumla wake vimechangia katika kushuka kwa ubora wa elimu na mafunzo nchini.


BOFIA HAPA KUPAKUA (DOWNLOAD) SERA YA ELIMU