UTANGULIZI
Baraza
la Taifa la Elimu ya Ufundi kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa wamefanya uchaguzi wa wanafunzi kwenye mafunzo ya Ualimu kwa
kozi za Stashahada ya Kawaida ya Elimu ya Msingi na Stashahada ya
Kawaida ya Elimu ya Sekondari Sayansi na Hisabati ambayo yataendeshwa
kwenye Chuo Kikuu cha Dodoma. Uchaguzi huu ni kwa wale wahitimu wa
kidato cha nne kwa mwaka 2014 waliofaulu kwa daraja la Krediti na zaidi
lakini hawakupangiwa kidato cha tano. Utaratibu wa kuripoti utatolewa na
chuo husika punde watakapomaliza maandalizi ya kupokea wanafunzi hawa.
Majina ya waliochaguliwa kujiunga na masomo kwa mwaka wa masomo
2015/2016 yameambatinishwa hapa.