NACTE - KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA PAMOJA WA UDAHILI KWA KIPINDI CHA MACHI/APRILI, 2017 KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017


NACTE - KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA PAMOJA WA UDAHILI KWA KIPINDI CHA MACHI / APRILI, 2017

 


TAARIFA KWA UMMA
 

KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA PAMOJA WA UDAHILI KWA KIPINDI CHA MACHI/APRILI, 2017 KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017 
NACTE (CAS Online) 2016/2017
NACTE (CAS Online) 2016/2017

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), linapenda kuutangazia Umma na wadau wote wa Elimu nchini, kuwa mfumo wa Udahili wa pamoja yaani Online Central Admission System (CAS), umefunguliwa rasmi tarehe 23 Januari, 2017, saa 6 mchana, kwa kupokea maombi ya mwombaji katika kozi mbalimbali, ikiwemo ngazi ya, Astashahada na Stashahada kwa Kipindi cha Machi/April, 2017 kwa mwaka wa masomo 2016/2017.
 
Namna ya Kufanya Maombi

Maombi yote yafanyike kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) au kupitia chuoni ambapo mwombaji anapendelea kwenda kusoma, ambapo chuo kitamdahili mwanafunzi husika kwenye mfumo wa udahili kupitia “Institutional Panel”.
Tanbihi: Waombaji wa kozi za Afya waliohitimu Astashahada (NTA Level 5), pia wataomba kwa utaratibu ulioelezwa hapo juu.
Mwombaji wa Astashahada na Stashahada anaweza kuomba kwa ajili ya eneo moja au zaidi katika maeneo ya taaluma yafuatayo:

  1. Biashara, Utalii na Mipango, mfano; Uhasibu, Meneja Rasilimali Watu, Wanyama Pori, Mipango.
  2. Sayansi na Teknolojia Shirikishi, mfano; Kilimo, Uhandisi, Mifumo ya Mawasiliano, Usanifu Majengo, Mifugo.
  3. Afya na Sayansi Shirikishi, mfano; Uganga, Maabara, Ufamasia, Uuguzi.
Sifa za muombaji

  1. Awe amehitimu kidato cha nne mwaka 2015 au kabla ya hapo.
  2. Awe na Astashahada ya mwaka 2016 au kabla ya hapo kwa wanaojiendeleza.
  3. Sifa kwa kozi mahsusi ziko kwenye mwongozo wa kozi (Guidebook) ulioko kwenye mfumo (CAS).
Ada ya maombi ni kama ifuatavyo:

  1. Kwa eneo la Afya na Sayansi Shirikishi ada ya maombi ni Tshs 30,000/=.
  2. Kwa eneo moja kati ya maeneo mengine yaliyobaki, ada ni Tshs 20,000/=.
  3. Kwa zaidi ya eneo moja la taaluma, mfano; Afya pamoja na Biashara, ada ni Tshs 30,000/=, ambapo muombaji anaruhusiwa kuchagua maeneo yote.
Mwisho wa kutuma maombi haya ni tarehe 06/03/2017.

Muhimu: Hakutakuwa na muda wa nyongeza wa kufanya maombi. Hivyo waombaji wanashauriwa kuwa makini wakati wa kufanya maombi yao.




Imetolewa na: 

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi

23 Januari, 2017

WHAT DOES IT TAKE TO BECOME A SUCCESSFUL STUDENT?

 

9 TIPS ON HOW TO SUCCEED IN YOUR EXAMS


Pata Matokeo Yote Ya Mitihani - One Spot For All The Examination Results New Updates (Kidato cha Pili na Darasa la Nne)

NACTE APPLICATION FEE PAYMENT PROCEDURE

APPLICATION FEE (Non refundable):
Application fee for this academic year are as in following categories:-
Which shall be paid through M-PESA using the following menu: Note: Payment Instructions: Please follow the steps below to pay through M-Pesa:
Payment Instructions Using Vodacom Mpesa: Malekezo ya Jinsi ya kulipia kwa Vodacom Mpesa:
  • 1. Dial *150*00#
  • 2. Select 4. Payments
  • 3. Select 4. Enter business number
  • 4. Enter the business number (607070)
  • 5. Enter reference No. (1234)
  • 6. Enter Amount (e.g 20,000/=)
  • 7. Enter PIN
  • 8. Press 1 to Confirm:
  • 1. Piga *150*00#
  • 2. Chagua 4. LIPA kwa M-Pesa
  • 3. Chagua 4. Weka namba ya kampuni
  • 4. Tafadhali weka namba ya kampuni No. (607070
  • 5. Weka namba ya kumbukumbu ya malipo No. (1234)
  • 6. Weka kiasi (e.g.20,000/=)
  • 7. Weka namba ya siri.
  • 8. Bonyeza 1 kuthibitisha:
After confirmation you will receive a message from Vodacom (e.g. "3GQ05BR3F4 28-07-2016 14:41:31 Pay bill to 607070 - NACTE acc. 1234 607070 - NACTE Completed TZS Tsh-20,000.00").
*Use the code at the beginning of the message to enter on payment details text box (3GQ05BR3F4).

Baada ya kutuma utapokeo ujumbe kutoka vodacom (Mfano "3GQ05BR3F4 Imethibitishwa. Tsh. 20,000 imetumwa kwa NACTE kwenye akaunti namba 1234 tarehe 26/7/16 saa 12:38 PM salio lako la M-PESA ni Tsh. 200").
*Tumia Uthibitisho wa malipo mwanzoni mwa ujumbe mfupi ulutumwa kutoka vodacom kuingiza kwenye kiboxi cha uthibitisho wa malipo (3GQ05BR3F4).

Payment Instructions Using Airtel Money: Malekezo ya Jinsi ya kulipia kwa Airtel Money:
  • 1. Dial *150*60#
  • 2. Select 5. Make Payments
  • 3. Select 3. Enter business Name
  • 4. Enter the business Name (607070)
  • 5. Enter Amount (e.g 20,000/=)
  • 6. Enter the reference Number. (1234)
  • 7. Enter PIN to confirm Paying 607070
    TShs 20000 with reference number 1234
  • 1. Piga *150*60#
  • 2. Chagua 5. Lipia Bili
  • 3. Chagua 3. Weka Jina la Kampuni
  • 4. Tafadhali Andika Jina La Biashara. (607070
  • 5. Ingiza Kiasi cha Pesa (e.g.20,000/=)
  • 6. Ingiza Namba ya kumbukumbu. (1234)
  • 7. Ingiza namba ya siri kulipia 607070,
    Tshs 20000 kumbukumbu rejea namba 1234.
You will receive a message from Airtel (e.g. " Txn Id: MP160506.0908.A07884 You have paid 20000.00Tshs to NACTE: Your available Airtel Money balance 200.00Tshs.").
*Use the Txn Id: (MP160506.0908.A07884,) to enter on payment details text box.

Baada ya kutuma utapokeo ujumbe kutoka Airtel (Mfano "Kitambulisho rejea: MP160506.0908.A07884, Umelipa 20000.00Tshs Kwenda NACTE.Salio lako jipya ni 200.00TShs.").
*Tumia Kitambulisho rejea: wa malipo (MP160506.0908.A07884) mwanzoni mwa ujumbe mfupi ulutumwa kutoka Airtel kuingiza kwenye kiboxi cha uthibitisho wa malipo.

NB: All applicants are advised to keep in safe place their confirmation number from Vodacom M-PESA payment or Txn Id from Airtel Money for future reference. Applicants are advised to read carefully the admission requirements of each programme they anticipate to apply in the guidebook before initializing the application process in order to avoid problems that may arise due to failure to follow appropriate instructions.

Career Guidance & Development To All Students